UEFA LEO VITA YA WAAFRIKA

In Michezo

Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi na mwenzake wa Tottenham Victor wanyama wamewekwa katika midomo ya Wakenya wengi wakati ambapo timu zao zitachuana katika kinyang’anyiro cha kombe la mabingwa mjini Madrid.

Nchini Kenya ambako raia wengi wanapenda soka , kuna matumaini kwamba wachezaji hao wawili wanaweza kung’ara na kuvutia maskauti katika taifa hilo la Afrika mashariki.

Huku mashabiki wa soka nchini Kenya wakisubiri kwa hamu na gamu michuano ya kombe la mataifa ya Afrika , kuna maoni tofauti kuhusiana na mchuano huo wa klabu bingwa Ulaya.

Hii ni mara ya kwanza wachezaji wawili walio na mizizi yao kutoka Kenya watashiriki katika fainali ya kombe la mabingwa .

Wanyama na Origi wataiwakilisha Kenya katika mchuano huo hatahivyo wakichezea timu tofauti.

Mashabiki wa soka katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakijadili ushindi wa timu ya Liverpool na Tottenham zinazotarajiwa kuminyamana katika fainali ya ligi ya mabingwa katika mji wa Madrid Uhispania.

Kuna shauku kubwa miongoni mwa Wakenya huku baadhi wakihoji kwamba fainali hiyo ni kama Derby ya ‘Mashemeji’.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MBUNGE JAGUAR WA KENYA ALIYETISHIA KUWAFURUSHA WATANZANIA AKAMATWA

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemkamata mbunge wa jimbo la Starehe anayedaiwa kutoa kauli za chuki dhidi ya wafanyabiashara

Read More...

MANCHESTER CITY, YAMTOA KAFARA DANILO

. . Klabu ya Manchester City, ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 44 na beki wao wa pembeni

Read More...

TOTTENHAM MBIONI KUMSAJILI KIUNGO KUTOKA LYON.

. . Klabu ya Tottenham, imekubali kutoa kitita cha kiasi cha paundi milioni 62 kumsajili kiungo wa kati wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu