Zaidi ya shilingi Bilion nane 8 zimetolewa na serikali ya uingereza ikishirikina na serikali ya Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji wa lita elfu tatu katika vijiji 5 vya Ngaramtoni, Seuri, Kilimamoto, Olkokola na Bangata vilivyopo halmashari ya wilaya ya Meru Mkoani Arusha
Akizungumza wakati wa ziara ya viongozi kutoka halmashauri 7 za mkoa wa Arusha wa ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo , mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ys Meru ambaye pia ni katibu wa jumuiya ya serikali za mitaa Charles Mahera amesema kuwa mradi huo wa maji utasaidia kupunguza changamoto ya ulemavu unaotokana na maji yenye madini ya floride
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Arumeru Bw,Noah Lembris amesema kuwa, mradi huo utakuwa msaada mkubwa kwa wananchi na unatarajiwa kukamilika mwezi wa 11 mwaka huu
Hata hivyo ziara hiyo imeanza leo ambapo kesho kitafanyika kikao cha majumuhisho kitakachojadili tathmini ya maswala ya maendeleo ya halmashauri 7 za mkoa wa Arusha ambazo ni Monduli, Longido, Ngorongoro, Meru Dc, Karatu, Arusha jiji, na Arusha DC