JUMLA ya nyumba 100 za makazi ya askari zimeanza kujengwa mkoani Dodoma, ikiwa ni mpango wa serikali kukabiliana na changamoto za makazi ya askari polisi
atakaohamia hivi karibuni baada ya serikali kuanza kutekeleza agizo la kuhamishia makao makuu ya nchi mkoani humo.
ayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na
salama kutembelea eneo la Medeli Mashariki ambako awamu ya kwanza ya mradi huo ukihusisha nyumba 30, ujenzi wa shule ya awali, ujenzi wa kantini, ujenzi wa
viwanja vya michezo tayari imeshaanza
“Ujenzi wa nyumba hizi unakwenda sambamba na ujenzi wa nyumba kama hizi katika maeneo mbalimbali nchini ili kuhakikisha askari wanaishi sehemu sa,”alisema.
libainisha kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha ujenzi wa nyumba kama hizo kote nchini unafanyika kwa gharama nafuu na kutumia wataalamu wa ujenzi waliopo
serikalini na katika Jeshi la Polisi.
“Mradi huu utakua na awamu tatu ambapo Aprili, mwaka jana, awamu ya kwanza ilianza na kutarajiwa kukamilika Aprili, mwaka huu, huku awamu zilizobakia zikitarajiwa
ukamilika mwisho wa mwaka huu na hadi kukia mwaka kesho katikati awamu zote zitakua zimekamilika,” aliongeza Masauni.
uku akishauri miradi mingine wajenge maghorofa ili kuweza kuitumia ardhi waipatayo kwa matumizi mengine sambamba na ujenzi wa makazi ya askari.
“Nawapongeza kwa kutumia mapato yenu wenyewe ya ndani kuanzisha miradi mikubwa kama hii na sisi wajumbe wa kamati tumeridhishwa na hatua hizi za kukabiliana
na makazi ya wapiganaji wetu wanaotulinda usiku na mchana na nchi yetu kuendelea kuwa na amani,” amesema.
jumla ya gharama ya mradi huo wa nyumba 100 za makazi ya askari polisi ni Sh bilioni 300.5 zinazotokana na Mfuko wa Tuzo na tozo ikiwemo malipo ya huduma
mbalimbali zinazotolewa na askari polisi na faini zinazotozwa na askari kwenye makosa mbalimbali.