Ujerumani yatoa Bil. 32.7 Kusaidia Afya Ya Mama Na Mtoto.

In Kitaifa
Ujerumani kupitia Benki yake ya Maendeleo (KFW) imeipatia Tanzania msaada wa Euro milioni 13, sawa na sh. bilioni 32.74 kwa ajili ya kuboresha afya ya uzazi na watoto wachanga na pia kukinga maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kupitia mradi ujulikanao kama Tumaini la Mama.
 Hafla ya utiaji saini mkataba wa msaada huo imefanyika Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James kwa niaba ya Tanzania na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani Dkt. Annika Calov.
 Msaada huo ni kwa ajili ya kutekeleza awamu ya tatu ya mradi huo unaotekelezwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambapo umelenga kuwapatia huduma akima mama na watoto wanaotoka katika kaya masikini
 Alisema kupitia mradi huo pia vifaa tiba vinavyohusiana na afya ya uzazi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi za Tanzania milioni 900 katika vituo vya Afya vilivyoko katika mikoa iliyochaguliwa kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa huduma za afya vimetolewa.
 Mradi huu ulianza mwaka 2012 ambapo Serikali ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kupitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) ilitoa Euro milioni 13 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 25.5 kupitia mkataba uliosainiwa tarehe 2 Desemba 2009.
“Awamu ya pili ya mradi ilianza mwaka 2016 ambapo Ujerumani ilitoa msaada wa Euro milioni 20 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 48.2 kupitia mkataba uliosainiwa tarehe 15 Machi 2015.  Siku ya leo Serikali yenu imeahidi kupitia mkataba huu, kutoa msaada mwingine wa Euro milioni 13 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 32.4 kutekeleza awamu ya tatu ya mradi, tunaishukuru sana,” alisema Bw. James.
James alisema mradi huo ni muhimu kwa kuzingatia kwamba unaongeza nguvu katika juhudi za Serikali za kupunguza vifo vya mama na mtoto lakini pia kuongeza tabia ya kutumia bima ya afya kwa watanzania na hii inaenda sambamba na awamu ya Pili ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano na awamu ya Tatu ya MKUZA.
“Kwa mfano, katika awamu ya Pili ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Serikali imelenga kwamba, hadi mwaka 2020:  Vifo vitokanavyo na uzazi vipungue kutoka 454 mwaka 2015 hadi 250 katika kila vizazi hai 100,000; muda wa kuishi uongezeke hadi miaka 66 kutoka miaka 56; na maambukizi ya VVU na UKIMWI yapungue kutoka asilimia 9 hadi 3,” alisema .
Naye Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani Dkt. Annika Calov alisema nchi yake inajivunia uhusiano mzuri na Tanzania na kwamba mradi huo wa Tumaini la Mama umelenga kuboresha afya akina mama wanaotoka katika familia maskini.
“Lengo kubwa ni kuboresha afya za mama na mtoto na kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kwa kuanzia mradi huu umekijita katika mikoa mitano ya Mbeya, Songwe, Tanga, Lindi na Mtwara,” alisema Calov.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bernard Konga alisema tangu mwaka 2012 mradi ulipoanza, jumla ya akinamama 1,157,191 wamenufaika na bima ya afya kupitia NHIF na kaya maskini 627,000 zimenufaika na huduma za CHF kwa kulipiwa ada za kujiunga.
“Akina mama na watoto wao wanapatiwa huduma kwa njia ya bima ya afya kupitia vituo vya afya 1097 vilivyoko katika mikoa hiyo iliyolengwa pamoja na mfuko kutoa vifaa tiba kwenye vituo,” alisema Konga.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu