Ujumbe wa mwisho wa Zari kabla ya kum-unfollow Diamond

In Burudani, Kitaifa
vi karibuni msanii wa nyimbo za Bongo fleva nchini, Naseeb Abdul maarufu duniani kama Diamond Platinumz amekuwa akiingia katika skendo za kuchepuka kimapenzi na baadhi ya mastaa mbalimbali hapa nchini akiwemo Tunda na Wema Sepetu.
Kufuatia matukio hayo mama watoto wa Diamond , Zarinah Hassan ameamua kuchukua uamuzi mgumu alioufanya kwa vitendo zaidi kuliko maneno kama ambavyo imezoeleka na kuacha maswali mengi kwa mashabiki wa wawili hao.
Wengi walitegemea kuona Zari akimlushia vijembe baba watoto wake kama ambavyo imekuwa kipindi cha nyuma Diamond alipopata skendo na Hamissa  Mobeto.
Zari kupitia akaunti yake ya instagram yenye wafuasi milion 3 na zaidi ameamua kumu-unfollow baba watoto wake, Diamond Platinumz kitu ambacho kimezua gumzo mtandaoni.
Ujumbe cha mwisho aliopost Zari kabla ya kuchukua uamuzi huo ulikuwa ni:
”There is no secret in life, whatever your Goals, you can get there if you are willing to work”, akimaanisha,
”Hakuna siri katika maisha, unaweza kufikia malengo ikiwa una nia ya kuyafikia, na kufikia malengo yako unatakiwa kuamua na kuwa tayari”. Alituma post hiyo January 30, 2018, siku ambayo Diamond na Wema Sepetu wakiwa stori kubwa ya siku baada ya kuonekana klabu pamoja.
Hayo yamejiri siku chache zilizopita wakati wa uzinduzi wa kumtambulisha rasmi Maromboso katika familia ya WCB, Wema Sepetu akiwa kama mgeni mwalikwa katika shughuli hiyo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Suzan Kiwanga afukuzwa Bungeni.

Spika wa Bunge, Job Ndugai jana alimtoa nje ya bunge, Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga (Chadema) na kumtaka kutohudhuria

Read More...

Mtolea ajivua Uanachama wa CUF Akiwa Ndani ya Bunge Leo.

Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea, kwa tiketi ya CUF ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge na nafasi zote ndani

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu