Unakumbuka nini ulivyokua mdogo?Kutengeneza manati na kuwinda

In Burudani

Naikumbuka michezo ya zamani ya watoto

Kutengeneza manati na kuwinda ndege porini,kuku wanaodonoa mahindi au
unga uloanikwa nk, shabaha ilikuwa Sifa muhimu kwa mmiliki wa silaha hii,
walioishi kwenye ngedere manati yalifaa sana kuwafurusha tumbiri wala mazao
kv mahindi na mpunga.
Kuunda magari ya waya yenye uwezo wa kupakia hadi kilo mbili, malighafi ilikuwa
ni waya za Tanesco au ttcl,mipira,fimbo yaani sterling rod,Bomba yaani deaf na
makandambili( ya Umoja ndo yalikuwa imara) usiweke Tairi za Bora sio imara.
Kidali poo, sikucheza sana Sina details zake:Kibabababa na kimamamama hapo
namkumbuka Mke wangu wa utotoni Khadija Mtengela(imagery ), tulilichukulia
kwa uzito ingawa ni utoto
Kushona makambakamba vidoleni na kuyachezesha kwa mitindo mbalimbali,huu
walicheza sana wadada.
Falsafa ya ujamaa ulikuwa mchezo muhimu sana, kwamba ukija na
kimbama,kisheti,gimbi au muwa marafiki zako lazima wapate.
Mkitoka Shule aliekuzingua skuli asiombe mvuke mpaka wa Shule muingie uraiani
hapo ni ngumi tu na kabla hamjaanza unachorwa mstari atakaeanza kurusha
ngumi anapata pointi ya ubabe kwa mwenzake…Basi ilikuwa ni vitisho ” subiri
kengere igonge utanijua labda ubadili njia…” Mkikutana mkazikunja utasikia “anza
wewee anza wewe…”
Mchezo wa kuzungusha pia. Tuliicharaza mijeredi inazunguka hadi inatoa
mlio,sanaa yake ya kipekee
Kupuliza kimhwepelo , unabana viganja vyote na kuvielekeza mdomoni kisha
unapuliza kupata milio mizuri
Kuzungusha magurudumu…Hapa kuna categories wababe walizungusha ya
Pigeot 504 au Hilux Datsun, wa kati Tairi ya pikipiki wadogo walikimbiza malingi ya
baiskeli kwa kutumia spoko maalum ambayo inakunjwa Fulani na kulipa lingi
mwendo kasi huku mwenyewe unalifukuza balaa
Tuliunda pikipiki zinazotoa mlio kwa kutumia makopo ya Dawa ya mlazo

Kuna wachache walipenda sana kucheza Yale mambo yetu sie tuliita ‘wanafanya
uchafu’ au ‘ wanafanya matusi_’ wapenzi wa mchezo huu walikuwa hawapendi
kujichanganya wao zao machakani
Tulicheza kwa Makundi makubwa na tuliagana kwa kombolela kitakaekulalia
kesho utaanzisha game
Soka chandimu tulikuwa vizuri zaidi tulipenda danadana,zubaisha bwege na
gombania goli
Pool sie tuliicheza tena sio asubuhi kwamba sirikali itatukamata mmh tukitoka
Shule wenyee tuliita ndula
Mchezo wa kujipikilisha

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WAGONJWA WA CORONA WAFIKIA 13 TANZANIA

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema idadi ya wagonjwa wa corona imefikia 13 ambapo kati yao 8 ni

Read More...

CORONA HAITAZUIA KUFANJIKA KWA UCHAGUZI – JPM

Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amesema Ugonjwa wa Corona hautaizuia Tanzania kufanya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Rais

Read More...

Mshtakiwa wa mauaji ya mfanyakazi wake wa Ndani, apandishwa kizimbani

Mshtakiwa wa mauaji ya mfanyakazi wake wa Ndani Mkami Shirima(30)Mkazi wa Sakina Arusha amefikishwa tena katika mahakama ya hakimu

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu