Uongozi wa Ubungo Plaza wazungumzia kufungwa kwa Blue Pearl.

In Kitaifa
Uongozi wa Ubungo Plaza Limited umesema mpangaji wake, hoteli ya Blue Pearl alikoma kulipa kodi ya pango tangu Mei, 2014.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Novemba 9,2017, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ubungo Plaza, Harun Mgude amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kushinda kesi Mahakama ya Ardhi.
“Blue Pearl amekuwa mpangaji wetu tangu mwaka 2006 na mkataba wake ulikuwa wa miaka 15 ambao ungeisha 2021. Alikuwa akilipa vizuri lakini tangu Mei 2014 aliacha kulipa,” amesema Mgude.
Amesema kutokana hilo walikwenda kufungua kesi Mahakama ya Ardhi na Blue Pearl wameshindwa, hivyo kutakiwa kulipa au kutoka ndani ya jengo.
“Kama mnakumbuka tuliwahi kumtoa na akarudi kwa amri ya Mahakama ili kupisha kesi kuendelea, lakini Novemba 3,2017 kesi iliisha na ameshindwa na kutakiwa kulipa deni la Sh5.7 bilioni,” amesema.
Amesema uongozi wa Blue Pearl umeomba kufanya kikao Jumatatu Novemba 13,2017 ili kujadili jinsi ya kulipa deni hilo.
“Baadhi ya wateja wamehamishiwa hoteli nyingine sijui ni wapi. Ila ieleweke kuwa robo tatu ya mali zilizokuwamo Blue Pearl ni za Ubungo Plaza Limited kama vile fenicha na vitu vingine,” amesema Mgude.
Uongozi wa hoteli hiyo ulikuwa ukishughulikia kuwahamisha wateja na haukuwa tayari kuzungumzia suala hilo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu