Upinzani Afrika kusini wataka Bunge livunjwe.

In Kimataifa

Chama kikuu cha upinzani nchini Afrika Kusini hapo jana kiliwasilisha hoja kikitaka bunge la nchi hiyo livunjwe na uchaguzi uitishwe mapema, ikiwa ni siku chache baada ya hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma kugonga mwamba.

Graham Charters, msemaji wa chama cha upinzani cha Democratic Alliance, amesema hoja hiyo mpya tayari imewasilishwa kwa spika wa bunge atakayeamua iwapo itapelekwa mbele ya bunge.

Zuma, mwenye umri wa miaka 75 ambaye kipindi chake cha pili na cha mwisho cha uongozi kinamalizika mwaka 2019, amenusurika mara kadhaa kuondolewa madarakani kupitia kura ya kutokuwa na imani naye iliyoitishwa kufuatia tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Hata hivyo, chama cha ANC hapo jana kiliapa kuikwamisha hoja hiyo kama kilivyowahi kukwamisha hoja nyingine kama hizo zenye lengo la kuiangusha serikali ya chama hicho.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu