Upinzani Congo wasema nchi hiyo haiko tayari kwa Uchaguzi.

In Kimataifa

Chama kikuu cha upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kimesema nchi hiyo haiko tayari kuandaa uchaguzi mkuu unaotarajiwa tarehe 23 Desemba, siku moja baada ya jeshi la nchi hiyo kukabidhi malori 150 na ndege kadhaa zitakazotumika na tume ya uchaguzi kusafirisha maafisa na vifaa vya kupigia kura. Msemaji wa chama cha Union and Social Progress-UDPS Augustin Kabuya amesema malori 150 hayatoshi kukidhia mahitaji ya usafirishaji wa vifaa vya kupigia kura katika taifa hilo kubwa kijiografia ambalo halina miundo mbinu mizuri ya barabara. Licha ya hayo, uchunguzi wa maoni ya wapiga kura uliotolewa jana unaonesha kuwa mgombea urais wa chama cha UDPS Felix Tshisekedi anaongoza kwa umaarufu kwa asilimia 36 akifuatiwa na Vital Khamere aliye na asilimia 17 huku mgombea urais wa chama tawala Emmanuel Ramazani Shadary anayeungwa mkono na Rais Joseph Kabila akiwa watatu na asilimia 16. Uchunguzi huo pia unaonesha kuwa theluthi mbili ya Wacongo wanaunga mkono wito wa kutaka chaguzi kucheleweshwa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Suzan Kiwanga afukuzwa Bungeni.

Spika wa Bunge, Job Ndugai jana alimtoa nje ya bunge, Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga (Chadema) na kumtaka kutohudhuria

Read More...

Mtolea ajivua Uanachama wa CUF Akiwa Ndani ya Bunge Leo.

Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea, kwa tiketi ya CUF ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge na nafasi zote ndani

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu