Utoaji chanjo ya Ebola waanza mjini Bikoro kaskazini magharibi ya Congo.

In Afya

Maafisa nchini Congo walianza jana kuwapa chanjo wafanyakazi wa afya na watu wengine katika eneo la Bikoro, ambalo mlipuko wa karibuni wa Ebola uliripotiwa kuanzia mapema mwezi Mei. Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kidekomrasia ya Congo Oly Ilunga alisafiri kwenda kusimamia zoezi hilo la utoaji chanjo kwa karibu watu 10 wa mji wa Bikoro, ambako karibu watu watano kati ya 12 waliofariki dunia kutokana na ugonjwa huo hatari walitokea eneo hilo. Kampeni ya utoaji chanjo ya Ebola nchini Congo, ambayo ilianzia mjini Mbandaka wiki iliyopita, inawalenga zaidi ya wahudumu wa afya 1,000. Zaidi ya watu 360 walipewa chanjo kabla ya jana Jumatatu. Mpaka jana, serikali ya Congo ilitoa takwimu mpya ikisema kuna visa 54 ya homa hiyo hatari ambapo 35 kati ya visa hivyo vimethibitishwa kuwa vya Ebola.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Majeshi ya Marekani yauwa raia Somalia

Majeshi ya Marekani yanayoendesha mashambulizi ya angani nchini Somalia dhidi ya ngome za wapiganaji wa Al Shabab nchini humo

Read More...

Idai yapoteza makazi ya watu 400,000.

Shirika la Msalaba Mwekundu linakadiria kuwa watu 400,000 wamepoteza makaazi yao nchini Msumbiji kutokana na Kimbunga Idai kilichoipiga nchi

Read More...

Baa la njaa kuikumba Kenya.

Zaidi ya watu milioni 1.5 nchini Kenya wako katika hatari ya kukabiliwa na baa la njaa kufuatia kutokuwepo kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu