Kenya imechaguliwa kuwa sehemu ya utafiti wa vidonge vya uzazi wa mpango kwa wanaume.
Nchi nyingine zinazoungana na Kenya ni Uingereza, Italia na Chile ambapo wanaume watatakiwa kunywa kidonge kimoja kila mwezi.
Taasisi ya Taifa ya Maendeleo ya Afya ya mtoto ilitengeneza kidonge kwa ajili ya kuwahimiza wanaume kutumia njia za uzazi wa mpango.
Inaelezwa kuwa mwanaume anayetumia kidonge anatarajiwa kupunguza idadi ya mbegu za kiume ndani ya saa 72 na kupunguza uwezekano wa kutungisha mimba.
Hili suala likifika Tanzania je unadhani wanaume watalipokeaje?