Vifo 800 vyaongezeka kwa siku moja Italia

In Kimataifa

Idadi ya vifo vinavyotokana na maambukizi ya virusi vya corona nchini humo inaongezeka kila uchao nchini Italia. Hadi kufikia jana Jumamosi watu 800 walikufa, na kuifanya idadi jumla kufika karibu watu 5,000 waliokufa kutokana na homa ya COVID 19 nchini humo. Kufuatia hali hiyo, serikali ya nchi hiyo imeamrisha biashara zote kufungwa hadi ifikapo Aprili 3. Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte amesema kupitia vidio iliyoruishwa kwenye mtandao wa Facebook kwamba wakati huu ni mbaya kuwahi kutokea tangu baada ya kumalizika vita vya dunia, na kuongeza kwamba shughuli za kibiashara zilizo muhimu ndizo zitaruhusiwa kuendelea kufanya kazi. Tangu Alhamisi iliyopita, Italia ilichukua nafasi ya kwanza na kuipita China kwa idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya virusi hivyo vya corona.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu