Viongozi wastaafu wahimiza amani barani Afrika.

In Kimataifa

Marais wastaafu Benjamin Mkapa wa Tanzania, Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia, wamezihamasisha serikali za Afrika, kugharimia shughuli za kulinda amani katika bara hili.

Walisema hayo Dar es Salaam jana kwenye mkutano wao na waandishi, walipozungumzia Kongamano la Kikanda la Viongozi Wastaafu Kuhusu Nafasi ya Afrika katika Mfumo wa Amani na Usalama Duniani, lililofanyika juzi. Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Uongozi. Uongozi ni taasisi ya serikali inayojitegemea. Walieleza kuwa hali ya amani na usalama Barani Afrika, inaendelea kukabiliwa na changamoto nyingi, hivyo viongozi wa Afrika wanatakiwa kuongeza juhudi za kuimarisha utengamano na uwezo wa kujenga na kulinda amani.

Mambo hayo ni kuimarisha taasisi za Kikanda na Umoja wa Afrika (AU), zenye jukumu la kujenga na kulinda amani; na Kuongeza uratibu, ushirikiano na mashauriano miongoni mwa taasisi za kitaifa, kikanda na bara zima, zinazohusika na juhudi za kuzuia migogoro na kulinda amani. Pia, kuimarisha mifumo ya ushirikiano baina ya Baraza la Amani na Usalama la AU na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) ili kuongeza sauti ya Afrika katika maamuzi ya UN kuhusu amani na usalama wa Afrika. Jambo lingine ni kuhakikisha nchi zote wanachama wa AU, zinajiunga na kutumia Mfumo wa Kujitathimini wa Afrika (APRM), kama chombo muhimu cha kuimarisha maridhiano ya kitaifa na kuzuia migogoro na uvunjifu wa amani; pamoja na Kuhamasisha serikali za Afrika kushiriki kugharimia shughuli za kulinda amani.

Mwandishi mmoja alitaka kujua kwa nini kongamano hilo, lilijadili nchi mbili tu za Somalia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambapo Mbeki alijibu kuwa “Kongamano lilijadili Somalia na DRC kwa kuwa ni mifano halisi inayotoa mafunzo kwa ajili ya mjadala kuhusu migogoro ya amani na usalama barani Afrika, na pia kwa sababu ya ufinyu wa muda.” Katibu Mtendaji wa Mkutano wa Kimataifa Juu ya Eneo la Maziwa Makuu, Balozi Zachary Muburi-Muita, aliyekaribishwa kwenye kongamano hilo la marais wastaafu, alisema “Matatizo ya kiafrika ni vema yatatuliwe kwa suluhu za kiafrika. Viongozi wa Afrika wasikae kitako kuona nchi zinawaka moto. Moto ukiwaka nchi moja hautaacha kwenda nchi jirani na kuichoma,” alisema Balozi Muita.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu