Kuna faida mbalimbali zitokanazo na matumizi ya vitamin kiafya hasa katika urembo
hususani katika vitamin C na Vitamin E ambazo huboresha muonekano wa ngozi yako.
Faida ya vitamin E katika ngozi hupunguza kasi ya ngozi kuzeeka, kupunguza madhara
ya mionzi ya jua kwenye ngozi lakini pia hupunguza muonekano mbaya wa makovu na
vipele.
Iwapo unataka kupunguza kupauka ngozi, madoa, makovu inashauriwa kuchanganya
mafuta ya Vitamin E na maji ya limao katika mafuta unayoyatumia pia unaweza
kuongeza rose water katika huo mchanganyiko.
Tumia pamba kupaka usoni na shingoni kaa na mchanganyiko huo kwa muda wa robo
saa kisha safisha uso tumia kwa siku 7 hadi 10 kuona mabadiliko pia itakusaidia kutibu
chunusi.
Unaweza kupaka usiku wakati wa kulala na asubuhi unasafisha uso wako kwa
kuchanganya kijiko kimoja cha ya mzaituni au mafuta ya nazi na mafuta kidonge kimoja
cha vitamini kisha unapaka kwa kuzunguka uso kwa kutumia vidole vyako.
Unashauriwa kutotumia mafuta ya Vitamin E bila ya kuchanganya na kitu chochote
kuyapunguza nguvu kunaweza kukuletea mchubuko wa ngozi laini kama ya kuzunguka
macho