Wabunge wa CCM wamwahidi ulinzi Rais Maguful.

In Kitaifa, Siasa

Rais Magufuli ameahidiwa  kupewa ulinzi kwa gharama yoyote ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi kwa sababu wanajua nia na dira ya wapi Rais huyo anataka kulipeleka taifa.

Ahadi hiyo ya ulinzi imetolewa na Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu kwa niaba ya wabunge wengine  ambapo amesema kuwa wao kama wabunge wa CCM wapo tayari kushughulika na chokochoko zinazofanywa na watu mbnalimbali kuathiri utendaji wa kiongozi huyo.

“Chokochoko za maneno zinazofanywa na watu ndani na nje ya chama, Wanasingida tunataka tukuhakikishe siyo wapiga kura wetu tu, hata kuku wetu hawatafanya maandamano. Hili ninakuhhakikishia kwa sababu mimi nikiwa kama Mbunge, na muwakilishi wa wananchi na na kiongozi ambaye ninayefahamu dira unayotaka kulipeleka taifa letu nataka nikuhakikishie utashinda vita hii,”Mh. Kingu.

Aliongeza ”Tutahakikisha mwenendo salama unaolinda heshima ya Rais ndani ya bunge na nje ya bunge, Chokochoko za upinzani ziko ndani ya uwezo wetu. Mh. Rais fanya kazi kwa ukitambua mbele yetu wewe,nyuma yako sisi.”

Aidha Kingu alisema kwamba Rais Magufuli anatakiwa kulindwa kwa sababu ameifuta nchi aibu kubwa ambayo mpaka mataifa madogo yalikuwa yakiicheka Tanzania, yeye ameifuta ikiwa ni pamoja na kufufua shirika la ndege lilokwa limekufa lakini pia kutekeleza miradi mikubwa kwa pesa kidogo tofauti na nchi jirani walivyotumia gharama kubwa katika miradi kama hiyo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Kitambulisho cha Vladimir Putin cha ujasusi chapatikana Ujerumani.

Kitambulisho cha Vladimir Putin alichopewa kama jasusi Ujerumani alipokuwa anafanya kazi kama jasusi wa Urusi kimepatikana katika makavazi mjini

Read More...

May aairisha kura kuhusu Brexit.

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ameahirisha kura iliyokuwa ifanyike leo bungeni kuhusu makubaliano ambayo serikali yake na Umoja

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu