WACHEZAJI WA MINZIRO WAPEWA SIKU 10 KULA BATA NA FAMILIA

In Michezo

UONGOZI wa Singida United umeamua kuwapa siku 10 za mapumziko wachezaji wake ili kurejea kwenye familia zao pamoja na kupata muda wa kupumzika kwa muda.

Singida United iliyo chini ya kocha Felix Minziro ilishindwa kubeba pointi tatu kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya KMC uliochezwa uwanja wa Namfua kwa kugawana pointi mojamoja.

Ofisa Habari wa Singida United, Cales Catemana amesema kuwa ligi imekuwa na ushindani hivyo wameamua kuwapa mapumziko wachezaji wapate akili mpya.

“Tunatambua kwa sasa bado mwenendo wetu haujawa mzuri ila bado tunapambana kurejea kwenye ubora, kwa sasa tumeamua kuwapa mapumziko ya siku 10 wachezaji ili wakirejea wawe na ari mpya.

“Mchezo wetu unaofuata ni dhidi ya Stand United ya Shinyanga hivyo baada ya kurejea kambini tutaanza kujipanga kwa ajili ya mchezo huo,” amesema

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MBUNGE JAGUAR WA KENYA ALIYETISHIA KUWAFURUSHA WATANZANIA AKAMATWA

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemkamata mbunge wa jimbo la Starehe anayedaiwa kutoa kauli za chuki dhidi ya wafanyabiashara

Read More...

MANCHESTER CITY, YAMTOA KAFARA DANILO

. . Klabu ya Manchester City, ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 44 na beki wao wa pembeni

Read More...

TOTTENHAM MBIONI KUMSAJILI KIUNGO KUTOKA LYON.

. . Klabu ya Tottenham, imekubali kutoa kitita cha kiasi cha paundi milioni 62 kumsajili kiungo wa kati wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu