Waendesha Michezo ya kubahatisha watakiwa kulipa kodi TRA.

In Kitaifa

Serikali imewataka waendesha michezo ya kubahatisha na wadau waliokua wakilipa kodi kwenye Bodi ya Michezo Tanzania (Gaming board of Tanzania) kulipa kodi na mawasilisho ya makusanyo yao kwa Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Hayo yamesemwa mapema hii leo jijini Dar es salaam na Kamishna wa kodi za ndani, Elijah Mwandumbya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, mbapo amesema kuwa kufuatia mabadiliko ya Sheria ya Fedha namba 4 ya mwaka 2017 yaliyofanywa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Sheria ya Michezo ya kubahatisha sura namba 166, TRA imepewa jukumu la kukadiria,kukusanya kodi kwenye michezo hiyo kuanzia Julai 1, mwaka huu.

Aidha, Mwandumbya amewataka walipaji kodi hao kuzingatia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja  na kusajili biashara hizo ili kupatiwa namba ya mlipakodi (TIN) kwa wasiosajiliwa

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo amesema kuwa kodi hiyo kwa waendeshaji michezo ya kubahatisha sio kitu kipya ila kilichobadilika ni mahali pa kulipia.

 

 

 

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu