Wafanyabiashara watakiwa kuhakikisha wanaweka mazingira katika hali ya usafi

In Kitaifa

HALMASHAURI ya jiji la Dodoma imesema,licha ya mikakati mbalimbali iliyoweka kwa wafanyabiashara wake,bado kuna Changamoto kadhaa zikiwemo kuziba kwa mitaro ya kupitisha maji na kurundikana kwa uchafu hasa wakati huu wa msimu wa mvua.


Kutokana na hilo wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao ndani ya jiji la Dodoma wametakiwa kuhakikisha wanaweka mazingira katika hali ya usafi katika Maeneo yao,na kuwa na vyombo Maalum vya kuhifadhia taka ili kuhakikisha afya ya walaji haidhuriki kutokana na uchafu.
Akizungumza na Radio 5 ofisini kwake Majengo Mkoani Dodoma Afisa Masoko wa halmashauri ya jiji hilo Bw,Jmaes Yuna amesema katika kipindi hiki cha msimui wa mvua halamsahuri hiyo kupitia kitengo cha masoko inahakikisha kuwa masoko yanakuwa safi kwaajili ya walaji.


,,Sisi tumejipangia utaratibu maalum wa kuhakikisha kuwa mazingira yetu yanakuwa safi katika msimu huu wa mvua na kuhakikisha mazingira yanayohusika na uwepo wa bidhaa ya walaji yanakuwa masafi ili kuwaepusha walaji na Maradhi Mbalimbali,,amesema yuna.
Amesema Mikakati,ni pamoja na kuhakikisha kuwa toroli zinazotumika kuzomba taka na kusafirishwa taka hadi katika Dampo la kisasa lililopo chidaya njia ya kuelekea mvumi wilayani Chamwino zinakuwepo wakati wote.
Amekiri kuwepo kwa changamoto Zinazoikabili Soko hilo ambapo ni miundombinu ya mitaro kuziba kutokana na taka zinaazosombwa na maji kutoka maeneo mbalimbali kipindi cha mvua,na kuwa wanazitatua kwa wakati ili wafanyabiashara wafanye kazi zao katika mazingira rafiki.


“ Zipo changamoto ndogondogo zinazosababishwa na mvua msimu huu,kutiririka kwa maji mengi,ila timu yetu inafanya kazi masaa yote ili kuhakikisha kuwa hilo linatatuliwa’’amesema.
Akizungumzia hatua mbalimbali zinazochukuliwa dhidi ya wale wanaokiuka kisheria amesema iwapo itabainika mtu yeyote kukiuka maelekezeo ya msingi kama kutupa taka kizembe ni kuwa atatozwa fedha hadi kiasi cha laki tatu ili kuhakikisha makosa hayo hayajirudii,na hilo ni katika kuhakikisha linakuwa funzo kwa wafanyabiashara.
Hivi sasa mkoa wa Dodoma kwa ujumla unashuhudia wimbi la wageni mbambali wakiwemo wafanyabiashara kutoka mikoa mbalimbali na hivyo kuna umuhimu wa kuyaweka mazingira katika hali ya usafi na salama ili kuepusha milipuko ya magonjwa yanayoweza kujitokeza.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Manchester City kushiriki kombe la Ulaya.

Klabu ya Manchester imefanikiwa kubadili marufuku ya miaka miwili kushiriki katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya kuanzia msimu

Read More...

Mama akiri kuua Watoto wake wanne.

Mwanamke mmoja nchini Kenya Betrice Mwende, anayeshikiliwa kwa tuhuma za kuwaua watoto wake wanne, amekiri Mahakamani kuwa ni

Read More...

Mtoto wa Nelson Mandela afariki dunia.

Zindzi Mandela, mtoto wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela na aliyekuwa balozi wa Afrika Kusini nchini

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu