Wahamiaji 15 wafariki dunia na wengine kumi kunusurika kifo katika pwani ya Libya

In Kimataifa

Wahamiaji 15 wamefariki dunia na wengine kumi kunusurika kifo kwa siku kumi na moja baharini baada ya boti lao kuzama katika pwani ya Libya. Kulingana na shirika la Hilali Nyekundu la Libya, wahamiaji hao walikuwa wanaondoka katika mji wa Sabratha ulioko magharibi mwa Tripoli kuelekea Italia lakini chombo chao kilipinduka na kuzama na kisha wahamiaji hao wakaogelea kwa kilomita 270 na kufika ufukweni. Kulingana na Baha al-Kawasha mbaye ni msemaji wa shirika hilo, hali mbaya ya hewa ilisababisha boti hilo kusukumwa na maji. Manusura hao kumi ambao kati yao ni wanawake wawili, walikuwa majini kwa siku kumi na moja bila chakula wala maji kabla kufika katika ufukwe Misrata hapo juzi Jumatatu. Kulingana na duru ambayo haikutaka kutambulishwa, wawili kati ya hao watu walioponea wanatokea Algeria na Misri kisha hao wengine wanane wanatokea nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Walikuwa na majeraha na ukosefu wa maji mwilini na walipewa huduma za kimatibabu kabla kupelekwa katika kituo cha kuwazuia wahamiaji Misrata.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tetesi za soka Ulaya.

Inter Milan wanafikiria kumnunua kiungo wa kati, Mfaransa N'Golo Kante huku Blues wakiwa tayari kusikiliza ofa kwa ajili

Read More...

Manchester City kushiriki kombe la Ulaya.

Klabu ya Manchester imefanikiwa kubadili marufuku ya miaka miwili kushiriki katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya kuanzia msimu

Read More...

Mama akiri kuua Watoto wake wanne.

Mwanamke mmoja nchini Kenya Betrice Mwende, anayeshikiliwa kwa tuhuma za kuwaua watoto wake wanne, amekiri Mahakamani kuwa ni

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu