Wakenya wamtafuta Rais Kenyatta katika mitandao ya kijamii

In Kimataifa

Wakenya wamekuwa wakitumia mtandao wa kijamii wa Twitter kuuliza maswali kuhusu mahali aliko rais wao Uhuru Kenyatta.

Bw. Kenyatta aliondoka nchi humo Aprili 23 kukutana na mwenzake Xi Jinping nchini China na inasadikiwa kuwa alirejea nyumbani kimya kimya Mey 3. Kwa mujibu wa gazeti la The Standard.

Kutoonekana hadharani kwa rais Kenyatta kumezua gumzo katika mitandao ya kijamii, huku wanasiasa wakipeana sababu tofauti kwa nini wanadhani raia ameamua kuwa kimya.

Gavana wa jimbo la Machakos lililopo nje kidogo ya mji mkuu wa Nairobi, Dr. Alfred Mutua alinukuliwa na vyombo vya habari akimtetea rais kwa kutoonekana hadharani kwa mda.

”Rais ni meneja mwenye shughuli nyingi kwa hiyo anahitaji mmda wa kufanya mikutano, kupokea taarifa muhimu za serikali na kushughulikia masuala ya uchumi wa nchi” alisema Bw. Mutua.

Aliongeza kuwa anashangaa kusikia watu wakiulizia kwanini rais hajaonekana hadharani tangu arejee kutoka ziara ya China.

Hata hivyo kupitia hashtag ya #FindPresidentUhuru, wakenya katika mtando wa kijamii wa Twitter maarufu KOT walituma ujumbe wa kutaka kujua rais Kenyatta yuko wapi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE

Real Madrid bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili Neymar, lakini wanataka hakikisho kutoka Paris St-Germain kuhusu hali

Read More...

(TAMISEMI) KUTOA TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani S Jafo kesho tarehe 23 Mwezi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu