Wakulima Wilayani Mbulu wameiomba serikali iwapelekee wataalamu.

In Kitaifa

Wakulima Wilayani Mbulu wameiomba serikali iwapelekee wataalamu wa kilimo na pembejeo za kutosha, ili kuwawezesha kuwa na kilimo chenye tija zaidi.

Ombi hilo limetolewa na umoja wa Wamwagiliaji wa Skimu ya umwagiliaji ya Mangisa iliyopo katika kata ya Dongobeshi, Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, walipokuwa wakizungumza na wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji walipoitembelea Skimu hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya umoja wa wakulima wa umwagiliaji, katibu wa umoja huo, Damiano Sulle, amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na wafadhili, ilifanya jambo la msingi kupeleka Skimu ya umwagiliaji katika eneo hilo ambapo ameeleza kuwa imeleta tija kwani ndio ajira pekee iliyo badilisha maisha ya wakazi wengi katika kata ya Dongobeshi.

Wameiomba serikali kuwasaidia kusakafia mfereji ambao haujasakafiwa wenye urefu wa mita 50, ambao utawasaidia wakulima kujipanga vizuri hasa katika matumizi sahihi ya maji, na kuongeza uzalishaji zaidi wa mazao.

Sambamba na hilo wakulima wameomba serikali kuwatafutia soko la uhakika hususani la zao la kitunguu swaumu, ili waweze kuuza zao hilo kwa mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani, kwani wana maghala makubwa ya kutosha ambapo wangeweza kuhifadhi mazao hayo na kuyauza wakati ambao bei za mazao hayo zikiwa juu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mgombea urais wa chama tawala Burundi atangazwa mshindi kwa kupata asilimia 68.7

Mgombea urais wa chama tawala nchini Burundi Evariste Ndayishimiye ametangazwa mshindi leo kwenye kinyang’anyiro hicho ambacho kimedaiwa kukumbwa

Read More...

Watu 7 Wanaodhaniwa Kuwa Majambazi Wauawa Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua majambazi saba na kufanikiwa kukamata silaha ndogo Bastola

Read More...

Watanzania watakiwa kucheki afya zao na kufuata ushauri wa daktari.

Watanzania wametakiwa kuwa na mazoea ya kwenda vituo vya afya kucheki afya zao na kuacha dhana ya kutumia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu