Walimu Kenya wataka kupatiwa bunduki kujilinda

In Kimataifa

Chama cha walimu nchini Kenya (KUPPET) kinaitaka serikali kutoa mafunzo ya usalama kwa walimu na kuwapa silaha wale wanaopelekwa kufundisha kwenye maeneo yaliyo ya hatari.

Kaimu Katibu Mkuu wa KUPPET Moses Nthurima amesema kuwapa walimu silaha si kuwa tu kutawaogopesha watu wanaowashambulia lakini pia kutawapa walimu hali ya kujiamini kufanya kazi katika mazingira ya hatari.

“Tunarudia ombi hilikwamba katika hali ya ukosefu wa usalama, lazima walimu wafundishwe na kupatiwa bunduki.”

”Huwezi kumkabili mtu mwenye bunduki kwa kutumia chaki. Tunapompeleka mwalimu katika maeneo ambayo usalama ni mbovu mwalimu ataishi kwa hofu kila wakati. Lakini ikiwa bunduki inaning’inia mgongoni hata majambazi watajua kuwa mwalimu ni eneo lisilofaa na watachukua sekunde kufikiri kabla ya kufanya makosa, “Alisema Bw. Nthurima.

Ombi hilo limekuja baada ya kutokea matukio ya kuuawa kwa walimu na watu wenye silaha katika maeneo ya Kaskazini-Mashariki na Pwani ya Kenya.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu