Wanafunzi wa shule ya msingi ya Kenyatta Golf Course Academy jijini Nairobi, waliwashangaza wengi baada ya kuyaweka madawati barabarani mapema leo na kusababisha msongamano mkubwa wa magari.

In Kimataifa

Wanafunzi wa shule ya msingi ya Kenyatta Golf Course Academy jijini Nairobi, waliwashangaza wengi baada ya kuyaweka madawati barabarani mapema leo na kusababisha msongamano mkubwa wa magari.

Wanafunzi hao, wakiwa kwenye sare zao rasmi za shule, waliimba na kujipanga kwa sehemu mbalimbali za barabara.

Walimu na wazazi wao nao walijiunga na wanafunzi wakiimba, “tunataka shule yetu, tunahitaji kutumia shule yetu”.

Shule hiyo inadaiwa kubomolewa wikendi kufuatia mzozo wa ardhi iliyotumika kujenga shule hiyo.

Wanafunzi hao wliondoka barabarani baadaye kwa hiari yao wakiwa na matumaini hali hiyo itasuluhishwa.

Zaidi ya shule elfu 24 za umma hazina hatimiliki ya ardhi zinazotumika na shule hizo na hilo limetajwa kutishia elimu ya watoto kwani shule 11,000 zimo hatarini kubomolewa au kunyakuliwa.

Maelfu ya watoto kutoka jamii maskini huenda wakakosa masomo kutokana na hali hiyo.

 

Walimu wa shule hiyo wameeleza wasiwasi wao kwani hatua hiyo imewaathiri kwa kuwaacha bila ajira

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu