Wananchi Ngorongoro waruhusiwa kujenga shule ndani ya hifadhi

In Kitaifa

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, uwaruhusu wananchi wa Kata ya Alaitole wajenge shule ya wasichana ya bweni katika eneo la Esere ,lililo ndani ya Mamlaka hiyo, ili waweze kupata elimu.

Ametoa agizo hilo kufuatia wananchi hao kuzuiwa kwa muda mrefu kutekeleza mradi huo, na kuutaka uongozi wa Mamlaka hiyo utoe kibali cha kuwawezesha wananchi kata hiyo, kuanza ujenzi haraka iwezekanavyo ili fedha zilizotolewa na Serikali shilingi milioni 298, zianze kutumika.

Dkt. Kigwangalla ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na kusikiliza kero za wananchi wa Kata Alaitole wilayani Ngorongoro ,kwenye mkutano wa hadhara uliowashirikisha viongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, viongozi wa serikali wa kata hiyo, viongozi wa mila wa kabila la Masai, madiwani na Mbunge wa jimbo la Ngorongoro Mhe. William Ole Nasha.

Hata hivyo Amesema Serikali inaunga mkono juhudi zote za wananchi za kujiletea maendeleo, na kwamba hatua ya wananchi hao kuamua kujenga shule ya Sekondari ya Bweni ,ni jambo la linalopaswa kupongezwa na kila mpenda maendeleo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MBUNGE JAGUAR WA KENYA ALIYETISHIA KUWAFURUSHA WATANZANIA AKAMATWA

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemkamata mbunge wa jimbo la Starehe anayedaiwa kutoa kauli za chuki dhidi ya wafanyabiashara

Read More...

MANCHESTER CITY, YAMTOA KAFARA DANILO

. . Klabu ya Manchester City, ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 44 na beki wao wa pembeni

Read More...

TOTTENHAM MBIONI KUMSAJILI KIUNGO KUTOKA LYON.

. . Klabu ya Tottenham, imekubali kutoa kitita cha kiasi cha paundi milioni 62 kumsajili kiungo wa kati wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu