Wanaotuhumiwa Kujiunganishia Bomba La Mafuta Wafikishwa Mahakamani

In Kitaifa
Watu saba akiwemo aliyekuwa fundi wa bomba la mafuta la Tazama, Samwel Nyakirang’ani (63) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka saba ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia bomba la mafuta.
Nyakirang’ani anashtakiwa pamoja na Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Ufukoni, Nyangi Matoro (54), Mfanyabiashara Farijia Ahmed (39), Malaki Mathias (39), Kristomsi Angelusi(25), Henry Fredrick (38) na fundi ujenzi Pamfili Nkoronko(40).
Washtakiwa walisomewa mashtaka yao jana mahakamani hapo na Wakili wa Serikali  Tulumanywa Majigo akisaidiana na Wakili wa Serikali Mkuu Peter Maugo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba.Wanadaiwa kutenda makosa yanayowakabili chini ya sheria ya uhujumu uchumi.
Akiwasomea hati ya mashtaka, Wakili Majigo alidai kuwa kosa la kwanza ni kujiunganishia isivyo halali katika bomba la mafuta ya Dizeli.
Imedaiwa, washtakiwa wote  katika tarehe tofauti kati ya mwaka 2015 na Januari 8, mwaka huu, huko maeneo ya Tungi Muungano katika Wilaya ya  Kigamboni jijini Dar es Salaam walijiunganishia bomba la upana wa inchi moja kwenye bomba la inchi 24 la  diesel material yasiyoshika kutu bila kuwa na kibali cha Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Katika shtaka jingine la kuharibu miundombinu ( kifaa kinachotumika kwa ajili ya utoaji huduma muhimu)  imedaiwa katika tarehe na maeneo hayo hayo, washtakiwa kwa pamoja walitoboa na kuharibu bomba la Inchi 24 linalotumika kusambaza mafuta ya Dizeli mali ya TPA.
Washtakiwa hao wanadaiwa pia kuwa, kati ya 2015 na January 8, 2018 maeneo ya Tungi Kigamboni, walitoboa bomba la inchi 28 la mafuta linalotumika kwa ajili ya usambazaji wa  Crude Oil likiwa ni mali ya TPA.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Wakili Majigo alidai Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amewasilisha hati ya kuzuia dhamana kwa washtakiwa hao.
Washtakiwa hawaruhusiwi kujibu lolote kwa kuwa kesi inayowakabili ni ya uhujumu Uchumi ma imeahirishwa hadi Januari 30,2018. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi bado haujakamilika, washtakiwa walirudishwa rumande.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu