Wanaume watakaotajwa kuwa ni wateja wa mashoga watakamatwa.

In Kitaifa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameunda kamati maalum ya watu 17 itakayoshughulika na masuala ya mapenzi ya jinsia moja jijini DSM kwa kile alichokieleza ni kukomesha biashara hiyo ndani ya Mkoa wa DSM.

Amesema miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo wanatoka TCRA Madaktari, Bodi ya filamu na wanasaikolojia.Makonda amesema hadi sasa amepokea msg 18,972 zenye majina ya ya zaidi ya watu 200 wanaofanya biashara ya ngono ya watu wa jinsia moja.

Kamati hiyo itashughulika na waigizaji wa filamu za ngono nchini, wamiliki wa nyumba zinazotumika kuigiza video za ngono, pamoja kuwatafuta watu wanaotumia mitandao kutapeli.

Makonda amezitaka mamlaka zinazohusika na haki za binadamu nchini kutoingilia suala hilo kwa kile alichokisema suala hilo ni kinyume na taratibu na sheria za Tanzania, amesema kwenye mkoa huo ushoga sio haki za binadamu ni kosa la jinai.

Makonda amesema baadhi ya mashoga wamefanya kazi hiyo kwa muda mrefu sasa wamechoka hivyo wanataka waache.

Ametoa wito kwa wakazi wa dar wafute picha za ngono kwenye simu zao kabla ya jumatatu. Makonda amesema wanaume watakaotajwa kuwa ni wateja wa mashoga watakamatwa, mashoga hao watapimwa na wte wawili watashitakiwa.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu