Washambuliaji wauwa wakristo sita kanisani Burkina Faso.

In Kimataifa

Watu wenye bunduki wamelivamia kanisa la kikatoliki katika mji wa Dablo nchini Burkina Faso na kuuwa watu sita jana Jumapili. Kulingana na duru za maafisa wa serikali, waumini walikuwa wakishiriki katika ibda ya asubuhi, wakati walipozingirwa na kundi la wavamizi takriban ishirini walioanza kuwafyatulia risasi. Washambuliaji hao walilichoma kanisa, kisha wakalitia moto duka moja na magari mawili. Mwezi Aprili, wakristo wengine 5 waliuawa katika shambulizi lililolenga kanisa la kiprotestanti katika mji mdogo wa Silgadji pia nchini Burkina Faso, mchungaji akiwa miongoni mwa wahanga. Miji ya Dablo na Silgadji iko Kaskazini mwa Burkina Faso, eneo ambalo limekuwa likiandamwa na mfululizo wa mashambulizi ya umwagaji damu, ambayo inaaminika yanafanywa na makundi ya kigeni yenye itikadi kali, yakiwemo Ansarul Islam, Kundi la Kulinda Waislamu na Uislamu-GSIM, na Dola la Kiislamu katika eneo la Sahara.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Baraka da Prince sasa kufunga ndoa na Naj

Msanii wa Bongo fleva Baraka de Prince amebainsha wazi kufunga ndoa mwaka huu na mpenzi wake Naj. Minong’ono ilikua

Read More...

Ajibuawataka Simba watulize boli, msimu ni wao

Nyota wa Simba, Ibrahim Ajibu amesema kuwa mashabiki wa Simba watulie watakubali mziki wake kwani amejipanga kufanya maajabu. Ajibu

Read More...

Waziri Mkuu kuzindua Daftari la kudumu la kupiga kura.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Dkt Athumani Kihamia, amesema zoezi la uandikishaji wa daftari la Kupiga

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu