WASHUKIWA WANNE MAUAJI HAITI WAUAWA

In Kimataifa

Jovenel Moïse aliuawa wakati washambuliaji walipovamia nyumba yake katika mji mkuu Port-au-PrinceImage caption: Jovenel Moïse aliuawa wakati washambuliaji walipovamia nyumba yake katika mji mkuu Port-au-Prince

Watu wanne wanaoshukiwa kumuua rais wa Haiti Jovenel Moïse wameuawa katika ufyatuaji risasi uliofanywa na vikosivya usalama, polisi imesema.

Wengine wawili wamekamatwa, huku washukiwa wengine waliosalia wakiaminiwa kuwa wamejificha katika mji mkuu -Port-au-Prince.

“Watauawa au kukamatwa,” mkuu wa polisi Leon Charles amesema.

Bw Moïse, aliyekuwa na umri wa miaka 53, aliuawa kwa kupigwa risasi na mke wake alijeruhiwa wakati washambuliaji walipoivamia nyumba yao mapema Jumatano.

Rais aliripotiwa kupigwa risasi nyingi na ofisi yake na chumba chake cha kulala viliporwa na kuharibiwa . Mke wa rais huyoMartine Moïse amesafirishwa kwa ndege hadiFlorida ambako anasemekana kuwa yuko katika hali mahututi lakini thabiti na anapokea matibabu.

“Mamluki wanne waliuawa na wawili wako chini ya udhibiti wetu,” Bw Charles alisema katika taarifa aliyoitoa kwenye televisheni siku ya Jumatano. “Polisi wawili waliokuwa wametekwa wamepatikana .”

“Tumewazuia washukiwa njiani walipokuwa wakiondoka kutoka kwenye eneo la uhalifu,” aliongeza. “Tangu wakati huo tumekuwa tukikabiliana .”

Kuna ongezeko la uwepo wa polisi karibu na makazi ambapo polisi waliuawaImage caption: Kuna ongezeko la uwepo wa polisi karibu na makazi ambapo polisi waliuawa

Aizungumza baada ya mauaji, Waziri mkuu Claude Joseph alitoa wito wa kuwepo kwa utulivu na alitangaza hali ya tahadhari kote nchini.

Hali ya tahadhari, inaruhusu kuzuiwa kwa mikusanyiko na matumizi ya jeshikwa polisi, na utekelezaji zaidi ya mamlaka.

Rais wa Marekani Joe Biden alitoa rambirambi kwa wtau wa Haiti kwa “mauaji ya kutisha “. Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson alikitaja kamakitendo “kinachoudhi ” na pia akatoa wito wa utulivu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu