Watu 18 Kupima DNA Kwa Makonda

In Kitaifa
Wanaume 18 kati ya waliofika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuhojiwa kuhusu kutelekeza watoto wamekubali kupimwa vinasaba (DNA) na Mkemia Mkuu wa Serikali, taarifa iliyotolewa jana na Paul Makonda ilisema.
Makonda alisema hatua hiyo imefikiwa na wanasheria na maofisa ustawi wa jamii baada ya kuhoji wanaume waliodaiwa kuwatelekeza watoto, katika malalamiko yanayoendelea kutolewa na wanawake kuanzia Jumatatu katika ofisi hizo, Ilala.
Mkuu wa Mkoa Makonda alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea maendeleo ya zoezi linalomalizika leo.
“Jumla ya wanaume 18 ambao walibisha kuwa watoto sio wao wamekubali kwenda kupimwa DNA kwa Mkemia Mkuu ili kupata uthibitisho wa uhalali wa mzazi na hao ni kati ya wanaume 198 walioitikia wito na kuja ofisini kwangu,” alisema Makonda.
Kadhalika, alisema kati ya wanaume 198 waliofika katika ofisi hizo baada ya kuandikiwa barua za wito, 179 walikubaliana na wanawake waliozaa nao mikakati ya kulea watoto husika.
“Familia 179 zimefikia muafaka,” alisema Makonda na “haya ni mafanikio makubwa. Kama watu waliokuwa hawahudumii familia na leo hii wamekubali kuhudumia na kurudi nyumbani kwa amani, kazi hii imezaa matunda.”
Makonda alisema kati ya wanaume 198 waliofika katika ofisi hizo kutafuta mwafaka, 19 kati yao mashauri yao yamepelekwa mahakamani ili kutafuta suluhu.
“Kazi inaendelea vizuri, tunaona mafanikio kwa sababu wanawake waliojitokeza ni wengi wanaokosa huduma kutoka kwa wanaume zao,” alisema. “Wanaume waliopewa barua za wito nao wamekuja wakasilikizwa na mwafaka ukapatikana.”
Pia alisema wanawake 1,498 wamejitokeza katika siku tatu kwa ajili ya kutoa malalamiko yao na kupewa msaada wa kisheria.Makonda alisema kutokana na kuwapo kwa idadi hiyo kubwa ya wanawake, wameongeza wanasheria 200 na maofisa ustawi wa jamii 60 na kusababisha kuwapo kwa watoa huduma 378.
“Kwa sababu ya mwitikio mkubwa wa wanawake, tumelazimika kuongeza wanasheria na maofisa ustawi wa jamii ili kazi hii ifanyike kwa haraka,” alisema Makonda.
Aidha, Makonda alisema baada ya kusikiliza wanawake waliotelekezwa, kanzia Jumatatu itakuwa zamu ya wanaume ambao wameandikiwa barua za wito.
“Ingawa wapo baadhi ya wanaume ambao wameandikiwa barua za wito na wameshakuja kusikiliza walichoitiwa, kuanzia Jumatatu itakuwa ni siku ya kuwasikiliza baada ya kuwasikiliza wanawake,” alisema Makonda.
Alisema wanaume ambao wamepewa wito huo wanatakiwa wajitokeze kusikiliza na endapo watakaidi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Makonda pia aliwataka wanawake na wanaume wenye matatizo ya kutelekezewa watoto kweli wajitokeze katika ofisi hizo ili wapate msaada wa kisheria bure badala ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii.
“Kama kweli mtu ana matatizo ni wajibu wake kuja hapa ili asikilizwe na kupatiwa msaada bure badala ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii ambako hakuna majibu,” alisema Makonda.
Leo ni siku ya mwisho ya kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake ambao walitelekezewa watoto na wanaume waliozaa nao.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu