Watu 479 wameuawa nchini kutokana na vitendo vya ukatili.

In Kitaifa

WATU 479 wameuawa nchini kutokana na vitendo vya ukatili ukiwamo wa watu kujichukulia sheria mkononi katika kipindi cha nusu mwaka 2017, ikiwa ni mara tatu ikilinganishwa na mwaka uliopita, jambo linaloonesha kuwapo ukiukwaji wa haki.

Aidha katika matukio hayo, Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa watu kujichukulia sheria mkononi kwa kuwa na matukio 117 yaliripotiwa polisi, ukifuatiwa na Mkoa wa Mbeya wenye matukio 33, Mara (28) na Geita (26).

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Helen Kijo Bisimba amebainisha hayo jana jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa ripoti ya hali ya haki za binadamu kwa kipindi cha nusu ya Mwaka 2017.

Ripoti hiyo inaonesha hali za binadamu kuwa bado ni mbaya kwa kipindi cha nusu mwaka ikilinganishwa na miaka iliyopita ambapo  Dk Bisimba amesema ripoti hiyo inayoanzia Januari hadi Juni mwaka huu ,inaonesha kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za kiraia hususani haki ya kuishi, lakini pia ukiukwaji mkubwa wa haki za makundi maalumu wakiwemo wanawake na watoto.

Amesema Jeshi la Polisi linapaswa kushughulikia haraka tatizo la kuwapo matukio hayo na kuhakikisha watuhumiwa wa matukio hayo wanafikishwa mbele ya sheria.

 

 

 

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu