Watu Takribani 29 wauawa Mashariki mwa DRC.

In Kimataifa

Takribani watu 29 wameuawa katika siku tatu za ghasia kati ya makundi yanayomiliki silaha katika eneo lenye utovu wa usalama mashariki mwa DRC,maafisa wamethibitisha.

Makundi mawili yanayomiliki silaha yanapambana kudhibiti kijiji cha Bweru katika jimbo la Kivu ya kaskazini,ambalo limekuwa likishuhudia umwagaji damu unaotakana na mapigano ya kikabila.

Kwa mujibu wa kiongozi wa eneo hilo Dieudonne Tshishiku,tangu siku ya jumatano makundi ya wapiganaji wa Mai mai Nyatura yamekabiliana kudhibiti kijiji na kusababisha vifo vya watu 29.

Kiongozi huyo amesema ghasia hizo bado zinaendelea katika kijiji cha Bweru na maeneo ya jirani na kulitaka jeshi la Congo kuingilia kati kukomesha vurugu na kuwarejesha raia waliokimbia makazi yao.

Afisa mmoja wa shirika lisilo la kiserikali amesema pasipo kutaja jina lake kuwa miongoni mwa watu 29 waliouawa ni wapiganaji 11 na kuongeza kuwa raia pia ni miongoni mwa waliouawa

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu