Watumishi wa Afya kuajiriwa kwa mkataba

In Kitaifa

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeamua kuanza kuajiri watumishi wa afya kwa mikataba wakiwemo wafamasia na wafamasia wasaidizi. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima alisema jana bungeni Dodoma kuwa, wamefanya uamuzi huo ili kukabili changamoto ya uhaba wa watumishi. Dk Gwajima aliyasema hayo wakati akijibu hoja za wabunge walizotoa wakati wakichangia bajeti ya wizara hiyo iliyowasilishwa bungeni) juzi.

“Wizara hii imeamua kujiongeza kwa kuajiri watumishi sekta ya afya kwa mikataba ambao wanaweza kulipwa mishahara nusu na mara nafasi za ajira zitakapopatikana watapewa ajira,” alisema. Dk Gwajima alisema upungufu wa watumishi ni tatizo kubwa katika wizara hiyo, na kwamba linachangiwa na watumishi takribani 2,800 wanaostaafu kila mwaka. Alisema wizara hiyo katika mwaka wa fedha 2021/22 iliomba kuajiri watumishi 13,000, lakini nafasi za ajira zilizotolewa serikali ni 2,726. Dk Gwajima alisema wizara imeandaa mwongozo ambao upo katika hatua nzuri katika ngazi za juu na ukipitishwa utasaidia wizara hiyo kupunguza upungufu wa watumishi kwa kutoa ajira za mikataba.

Alisema mwongozo ukipitishwa watumishi watapewa mikataba ya mwaka au zaidi, watapewa mshahara nusu, lakini kadiri fedha zinapopatikana watakuwa wakipewa kipaumbele kupewa ajira. “Haitawezekana kuajiri watumishi asilimia 100 na haijawahi kutokea katika nchi yoyote duniani, lakini kwa kupitia ubunifu huo wa wizara, mwongozo huo ukipitishwa wizara itaajiri watumishi hao kwa mikataba na itapunguza idadi ya wasomi wa sekta hiyo waliopo mitaani bila ajira,” alisema Dk Gwajima. Alisema, katika ajira hizo wizara itatoa kipaumbele kwa kuajiri watalaamu wakiwemo wafamasia na wasaidizi wao ili kutoa huduma bora kwa wananchi. Kwa mujibu wa Gwajima, ili kufanikisha hilo, pia wanaomba ushirikiano wa Ofisi ya Rais- Utumishi ili kutoa vibali kwa ajili ya kuajiri watumishi hao kwa kuwa wapo mitaani. Kuhusu tatizo la wizi wa dawa, alisema, serikali imechukua hatua kwa watendaji waliojihusika na vitendo hivyo na wamewakabidhi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Kuhusu watendaji kuonekana wachache katika baadhi ya maeneo, alisema wizara itachunguza kubaini maeneo yenye uhaba na kusambaza wahudumu kutoka kwenye maeneo walipo wengi. Kuhusu madeni kwenye Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Dk Gwajima alisema hadi Aprili mwaka huu, serikali imelipa Sh bilioni 16.3 na kubaki Sh bilioni 260.7. Alisema, katika kudhibiti mapato, serikali itaendelea kufunga mitambo ya Tehama katika vituo na kwamba, hadi sasa kitaifa ipo saba kwenye mikoa 14 na katika halmashauri 971. Dk Gwajima alisema mfumo huo utasaidia kubainisha namna dawa zinavyotolewa na itaonesha kama daktari ametoa makopo 20 ya ‘panadol’ badala ya mawili anayotakiwa kutoa kwa wagonjwa kwa siku

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu