WAZIRI LUKUVI AWATEUA WENYEVITI WA MABARAZA YA ARDHI.

In Kitaifa

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameteua wenyeviti 20 wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba na wengine 42 kupangiwa vituo kwa lengo la kuboresha na kuleta ufanisi katika mabaraza hayo.

Waziri Lukuvi amefanya uteuzi na mabadiliko hayo kutokana na mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Kifungu cha 25 (1) cha Sheria ya Mahakama za Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi, Sura 216.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, wenyeviti wapya 20 walioteuliwa ni Rajabu Mnyukwa mwenyekiti wa baraza Kilosa, Edward Mhina Nzega, Nadhiru Ngukulike Tarime, Rebeca Mjanja Lindi, Hussein Lukeha Mtwara, Augustine Lugome Kyela, Baraka Shuma Iramba na Tendai Chinolo
Lushoto.

Wengine walioteuliwa ni Mtengeti Sangiwa mwenyekiti wa baraza Njombe, Jackson Kanyerinyeri Maswa, Jacob Rungwe, Ntumengwa Ntumengwa Mbulu, Justina Lwezaura Rukwa, Jesca Mugalu Mbinga, Reginald Mtei Bukoba, Jimson Mwankenja Morogoro, Bahati Ndambo Chato, Richard Mmbando Ulanga, Felix Frederick Mpanda
na Ngassa Maduhu.

Uteuzi wa wenyeviti wa mabaraza ya ardhi na nyumba wa wilaya ni wa miaka mitatu kuanzia Aprili Mosi, mwaka huu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mgombea urais wa chama tawala Burundi atangazwa mshindi kwa kupata asilimia 68.7

Mgombea urais wa chama tawala nchini Burundi Evariste Ndayishimiye ametangazwa mshindi leo kwenye kinyang’anyiro hicho ambacho kimedaiwa kukumbwa

Read More...

Watu 7 Wanaodhaniwa Kuwa Majambazi Wauawa Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua majambazi saba na kufanikiwa kukamata silaha ndogo Bastola

Read More...

Watanzania watakiwa kucheki afya zao na kufuata ushauri wa daktari.

Watanzania wametakiwa kuwa na mazoea ya kwenda vituo vya afya kucheki afya zao na kuacha dhana ya kutumia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu