WAZIRI MKUU AONGOZA MAZIKO YA ASKOFU MMOLE.

In Kitaifa

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania kumuenzi Askofu mstaafu, Gabriel Mmole (80) wa Jimbo Katoliki Mtwara kwa wema, upole na utumishi
mwema wakati wote wa maisha yake.

Alitoa mwito huo jana wakati wa maziko ya askofu huyo yaliyofanyika ndani ya Kanisa la Watakatifu Wote la mjini Mtwara na kuhudhuriwa na viongozi, waumini wa Kanisa
Katoliki pamoja na wakazi wa mkoa wa Mtwara Katika Ibada ya maziko iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea, Mhashamu Askofu Damian Dallu, Waziri Mkuu
alitumia muda huo kuwaasa Watanzania kuishi katika maadili mema na kuheshimiana.

Waziri Mkuu amesema enzi za uhai wake Askofu Mmole alitoa kipaumbele katika masuala muhimu ya maendeleo ya jamii ikiwemo elimu ambapo alisaidia sana watawa
waliomaliza darasa la saba na kuwasaidia wajiunge na shule za sekondari. “Hata uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha STEMMUCO ambacho ni tawi la SAUT hapa Mtwara ni
moja ya jitihada zake alizozifanya katika kuhakikisha anawapa elimu bora vijana na jamii.
Askofu Mmole alizaliwa Januari Mosi, 1939 katika Parokia ya Nangoo, ambapo alibatizwa na kupata kipaimara Oktoba 5, 1952. Mwaka 1971 alipata daraja ya upadre na kuwa Askofu kuanzia mwaka 1988, alifariki Mei 15, 2019 mkoani Mtwara baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa aliwashukuru viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini mkoani Mtwara kutokana kwa ushirikiano mzuri anaopata
unaomwezesha kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Maziko hayo yamehudhuriwa na maelfu ya wananchi, maaskofu wa majimbo mbalimbali nchini, Rais Mstaafu wa
awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na mkewe, Mama Anna, Waziri wa Nchi Osi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Miss Tanzania Mikononi mwa Waziri Mkuu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka mshindi wa shindano la urembo Tanzania (Miss Tanzania) kwa mwaka 2019 Sylivia Bebwa, kuhakikisha

Read More...

Magufuli ampandisha cheo Brigedia Jenerali Charles Mbuge.

Rais Magufuli amemteua Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa JKT. Mbuge anachukua nafasi Meja Jenerali Martin Busungu ambaye

Read More...

SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE.

Juventus imekataa kumuuza winga Douglas Costa 28 licha ya Man United kuwa na hamu ya kumsajili baada ya mkufunzi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu