Waziri  Mkuu apokea maandamano ya wafanyakazi wakimpongeza Rais.

In Kitaifa

Waziri  Mkuu apokea maandamano ya wafanyakazi wakimpongeza Rais

SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Na limeyataka makundi ya wanasiasa kutowatumia wao kama njia ya kujitafutia umaarufu, kwa kuzungumzia masuala yao na badala yake wawaachie viongozi wa vyama hivyo kwa sababu wanajitosheleza.

Pia shirikisho hilo limesema litaendelea kuiunga mkono na kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano, pamoja na Rais wake Dkt. John Magufuli na kwamba watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia masharti ya Ajira zao.

Hayo yamesemwa  na Katibu Mkuu wa TUCTA, Yahya Msigwa katika hotuba yake aliyoitoa kwa wafanyakazi baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kupokea maandamano ya amani ya vyama vya wafanyakazi.

Katibu huyo wa TUCTA amesema mara nyingine makundi ya wanasiasa yamekuwa yakisema maneno ambayo wao hawajayasema, jambo ambalo limekuwa likiwachonganisha na wadau wao wakiwemo wanachama pamoja na Serikali.

Hata hivyo ameiomba Serikali ifanye uchunguzi kwenye miradi inayotekelezwa na mifuko ya hifadhi ya jamii, kwa sababu hawana uhakika kama miradi hiyo imerejesha fedha.

Pia amesema  suala la kupandisha mishahara, madaraja  na maslahi ya wafanyakazi kwa ujumla, Waziri Mkuu amesema  Rais Dkt. Magufuli alishalitolea maelekezo na kwamba Serikali inayafanyia kazi maelekezo yake, hivyo amewaomba wafanyakazi waendelee kuwa wavumilivu.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kulipa stahiki za watumishi wa umma kwa wakati  na kulipa madeni hatua kwa hatua,ambapo kati ya Julai 2018 hadi Septemba 2018, Serikali imelipa sh. bilioni 184.9 za madai mbalimbali ya watumishi

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Majeshi ya Marekani yauwa raia Somalia

Majeshi ya Marekani yanayoendesha mashambulizi ya angani nchini Somalia dhidi ya ngome za wapiganaji wa Al Shabab nchini humo

Read More...

Idai yapoteza makazi ya watu 400,000.

Shirika la Msalaba Mwekundu linakadiria kuwa watu 400,000 wamepoteza makaazi yao nchini Msumbiji kutokana na Kimbunga Idai kilichoipiga nchi

Read More...

Baa la njaa kuikumba Kenya.

Zaidi ya watu milioni 1.5 nchini Kenya wako katika hatari ya kukabiliwa na baa la njaa kufuatia kutokuwepo kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu