Waziri Mkuu Atoa Milioni 5 Kwa Mjasiriamali Mlemavu

In Kitaifa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemkabidhi Bibi Tecla Hamidu ambaye ni mlemavu wa miguu sh. milioni tano ili aweze kuongezea katika mtaji wake.
Ametoa fedha hizo leo (Jumanne, Machi 20, 2018) ikiwa ni katika kutimiza ahadi yake aliyoitoa Februari 22, 2018 kwenye Mkutano wa Sita wa Wamiliki wa Viwanda na Watumiaji wa simbomilia (barcodes).
Waziri Mkuu alitoa ahadi hiyo baada ya Bibi Tecla ambaye ni mjasiriamali anayejihusisha na ushonaji wa bidhaa mbalimbali zikiwemo nguo kumuomba amchangie sh. 500,000 ili aweze kuongezea mtaji wake.
Wakati akimkabidhi fedha hizo, Waziri Mkuu amesema kwamba anatarajia zitamsaidia katika kuongeza  mtaji wake, hivyo atazalisha bidhaa nyingi zenye ubora unaohitajika katika masoko ya ndani na nje.
Kwa upande wake, Bibi Tecla alimshukuru Waziri Mkuu kwa msaada huo na ameahidi kuzitumia fedha hizo kama ilivyo kusudiwa.
“Nashukuru kwa msaada huu kwani kuna watu wanakopa sh. laki mbili ili waongeze mitaji, lakini mimi leo nimepewa milioni tano bure na kiongozi wetu,”
Amesema licha ya kukabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa masoko anaamini tatizo hilo litakuwa historia baada ya kuwa na mtaji wa kutosha kwani atakwenda kuzalisha bidhaa zenye ubora zaidi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu