Waziri Mkuu Haiti ameahidi uchaguzi wa mapema

In Kimataifa

Waziri Mkuu mpya wa Haiti, Ariel Henry ameahidi kufanyika uchaguzi wa haraka wa taifa hilo, kufuatia kuuwawa kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo, Jovenel Moise.Henry amesema mpango wa serikali yake ni kufanikisha uchaguzi huru, wa kuaminika, wenye uwazi ambao utawashirikisha wapiga kura huku akisisitiza hitaji la usalama nchini humo.Lakini pia amezungumzia takwa la kukabiliana na tatizo la ajira na kuujengea uwezo mfumo wa kimahakama wa nchi hiyo na kuongheza amekutana na viongozi wa asasi za kiraia tangu ale kiapo chake Julai 20.Mkutano huo ambao umedumu kwa takribani dakika 10, umefanyika katika kipindi cha tofauti ya masaa machache baada ya Henry kukutana na baraza lake jipya la mawaziri katika mkutano wa ndani. Katika mkutano huo, inatajwa kwamba alitoa taarifa ya maendeleo ya uchunguzi wa mauwaji ya Julai, 7 ya Rais Moise. Kiongozi huyo aliwawa akiwa katika makazi yake binafsi kwenye mkasa ambao pia mke wake alijeruhiwa vibaya.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tetesi za Soka Ulaya leo Alhamisi Septemba 23, 2021

Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, hana hamu ya kusaini kandarasi mpya klabuni hapo. Mkataba wake wa

Read More...

Wanaharakati wa haki za binadamu wahoji hukumu dhidi ya Rusesabagina

 Makundi ya kutetea haki za binadamu barani Afrika yamelalamikia uamuzi wa mahakama kuu ya Rwanda ya kumfunga jela kwa miaka 25, Paul Rusesabagina ambaye alisifika sana kwenye filamu ya Hollywood ya Hotel Rwanda.  Mahakama hiyo Jumatatu ilisema kwamba imepata Rusesabagina pamoja na washukiwa wengine 20 na hatia ya

Read More...

LISSU NA WENZAKE WAFUTIWA KESI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeifutia kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu