WCB kuzindua televisheni na redio februari mwaka huu.

In Burudani, Kitaifa
Kampuni ya Wasafi Classic (WCB), inayomilikiwa na msanii maarufu wa muziki wa Bongofleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ wanatarajia kufungua televisheni na redio Februari mwaka huu.
Haya yamebainika ikiwa ni saa chache tangu Diamond na viongozi wa kampuni hiyo watupie jumba la kifahari  ambalo linaelezwa  litakuwa ndiyo  makao makuu ya WCB ambapo mbali ya kuwa na studio za kurekodia muziki pia litakuwa na Redio na TV.
Katika mahojiano hayo, Fela amesema hatua waliofikia ni katika harakati za kampuni hiyo kuendelea kujitanua na kutoa fursa kwa vijana wengi zaidi.
Meneja wa Diamond, Said Fela  amesema pamoja na kwamba wao ni watu wanaojishughulisha na kazi za burudani, lakini TV yao na redio zitakuwa zinarusha vipindi vya aina zote vikiwemo vya kuelimisha na habari kama vilivyo vituo vingine.
“Kwetu sisi hii tunaona ni hatua nzuri kwa kuwa tunajua tukifungua vituo hivi ndivyo kadri tunavyozidi kuzalisha ajira na tumeamua kutumia wataalam ambao walikuwa kwenye fani hiyo ikiwemo wazee waliostaafu katika Shirika la Utangazaji(TBC) enzi hizo TVT kwa ajili ya kutuongoza kwa kuwa sisi wenyewe hatuwezi,”amesema Fela.
Hata hivyo, alipoulizwa kama wamejenga wenyewe mjengo huo au Fela amesema wamekodisha kama walivyokuwa wamekodisha ile ya Sinza huku sababu za kuhama akieleza ni kutokana na kuongeza huduma na pia sehemu waliyokuwepo kulikuwa na taabu ya maegesho ya magari na kujaa maji hasa mvua zinaponyesha.
Mjengo huo wa wasafi wa ghorofa moja ambao upo maeneo ya Mbezi umeonekana kuwa gumzo  katika mitandao ya kijamii na watu wengi wamempongeza Diomond na uongozi wake kwa hatua aliofikia.
Mbali na redio, tayari Diamond ameshajiingiza katika biashara nyingine ikiwemo ya manukato yanayoitwa ‘Chibu’, na ‘Diamond karanga’

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu