The Weeknd atoa onyo kwa Wizkid na wasanii wengine wanaotumia neno ‘StarBoy.

In Burudani, Kimataifa

Msanii wa muziki kutoka Canada, The Weeknd amewaonya wasanii wa muziki dunia akiwemo Wizkid kuacha mara moja kutumia neno ‘StarBoy’ kwa madai kuwa neno hilo ameshalilipia (TradeMark) kwa matumizi yake ya kibiashara.

The Weeknd na Wizkid

The Weekend amesema kuwa yeye ndiye muanzilishi wa neno hilo ‘StarBoy’ na yeyote atakayetumia atachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Tayari wanasheria wa The Weeknd wameshaandaa nyaraka za kumburuza Eymun Talasazan mahakamani kwa kutumia neno ‘StarBoy’ kwenye vipindi vyake vya TV baada ya The Weeknd kuachia album yake ya ‘StarBoy’ mwaka 2016.

Wimbo wa ‘StarBoy’ ni moja ya nyimbo zilizopo kwenye album hiyo na ulifanikiwa kushika namba moja kwenye chati za Billboard top 100.

Kwa The Weeknd wimbo wa StarBoy ni wimbo wa tatu kushika namba moja kwenye chati hizo maarufu zaidi duniani.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

PICHA:Rais Magufuli akitoa salamu za pole familia ya Kikwete

Kufuatia kifo cha Rashid Mkwachu ambaye ni Baba mzazi wa mke wa Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, mama Salma

Read More...

Lugola awapa maagizo wakuu wa majeshi, Wafungwa watumie nguvu zao kujitaftia chakula.

Waziri wa mambo ya Ndani, Kangi Lugola mapema leo hii ameongea na vyombo vya habari akiwasilisha maagizo mbalimbali ambayo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu