Wema atoka mahabusu, Hakimu amuonya.

In Kitaifa

Msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu aliyekuwa mahabusu katika Gereza la Segerea ameachiwa kwa onyo na dhamana yake inaendelea.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Juni 24, saa nne asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde.

Akitoa uamuzi wa aidha Wema afutiwe dhamana au la, Hakimu Kasonde amesema kazingatia kiapo kilichowasilishwa na Wakili Albert Msando na maelekezo ya mshtakiwa lakini mahakama inaona ni kweli alivunja masharti ya dhamana.

Amesema sababu kubwa ni kuumwa ghafla ambapo alitakiwa siku ile ile angefika mahakamani kutoa taarifa si kuamua kuondoka.

“Mahakama inakuonya, uhakikishe pale ambapo haupo mahakamani, Mahakama ijulishwe kupitia mdhamini wako na si vinginevyo,” amesema Hakimu Kasonde.

Hakimu Kasonde amesema kosa hilo likijirudia Mahakama haitasita kumfutia dhamana.

Wema alienda gerezani Juni 17 mwaka huu, ambapo anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani.

Juni 11 mwaka huu Mahakama ilitoa hati ya kumkamata Wema kwa kosa la kuruka dhamana.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Baraka da Prince sasa kufunga ndoa na Naj

Msanii wa Bongo fleva Baraka de Prince amebainsha wazi kufunga ndoa mwaka huu na mpenzi wake Naj. Minong’ono ilikua

Read More...

Ajibuawataka Simba watulize boli, msimu ni wao

Nyota wa Simba, Ibrahim Ajibu amesema kuwa mashabiki wa Simba watulie watakubali mziki wake kwani amejipanga kufanya maajabu. Ajibu

Read More...

Waziri Mkuu kuzindua Daftari la kudumu la kupiga kura.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Dkt Athumani Kihamia, amesema zoezi la uandikishaji wa daftari la Kupiga

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu