West Ham, Everton na Burnley zamnyatia Samatta

In Michezo

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta anang’ang’aniwa na klabu tatu za England, taarifa za vyombo vya habari nchini Uingereza zinasema.

Tetesi zinasema nyota huyo anatafutwa na West Ham United, Everton na Burnley.

Samatta, 25, maarufu kwa Watanzania kama Samagoal ameng’aa sana akichezea klabu ya KRC Genk nchini Ubelgiji.

Amefungia klabu hiyo mabao 11 katika mechi 16 ambazo amewachezea msimu huu, nusu ya mabao hayo akiyafunga barani Ulaya.

Taarifa za kumhusisha Samatta na klabu ya Everton zimetoka kwa mtandao wa hitc.com, mmoja wa mitandao ambayo imeibukia kuwa maarufu kwa taarifa za wachezaji na kuhama kwao.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Familia Ya Mo Dewji Yatangaza mkwanja wa Bilioni 1 (1,000,000,000) kumpata Mo.

Familia ya Mfanyabiashara wa Tanzania Mohammed Dewji imetangaza zawadi nono ya TSH. BILIONI MOJA (1,000,000,000)  kwa yeyote atakaetoa taarifa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu