Wilaya ya Mwanga kuboresha miundombinu ya mabwawa na misitu

In Kitaifa

Mwanga.Serikali ya wilaya ya Mwanga  Mkoani Kilimanjaro imeanzisha mpango endelevu wa kuboresha miundombinu ya mabwawa na misitu ya asili iliyopo katika wilaya hiyo ili kuwa raslimali zitakazoinua kipato cha wananchi na Halmashauri ya wilaya hiyo.


Mkuu wa  Wilaya ya Mwanga,Thomas Apson ameyasema May 19,2020  mara baada ya kutembelea bwawa la Chunguli(Kisanjuni) lililopo Tarafa ya Ugweno wilayani humo.
Aidha amesemaema kuwa,Wilaya hiyo imepanga mkakati wa kuboresha bwawa la Nyumba ya Mungu ambalo ndio chanzo kikubwa cha  ukusanyaji wa mapato katika  Halmashauri hiyo pamoja na kulifufua bwawa la Kisanjuni na ziwa jipe.
Apson amesema Wilaya ya Mwanga wamepanga kuboresha bwawa la nyumba ya Mungu,ziwa jipe,bwawa la kisanjuni pamoja na kufanya mradi mkubwa wa ufugaji nyuki katika misitu ya kileo na kambi ya nyani .


Amesemama Bwawa la Kisanjuni ambalo lilisahaulika kwa muda mrefu litafufuliwa upya kwa kutengeneza fursa mpya ya uvuvi ili kukuza ajira kwa vijana na kukusanya mapato mapya ya Halmashauri hiyo na kusema watafanya kila namna ili kuhakikisha wilaya hiyo inaboreka kimapato.

Naye Mhadhiri Mkuu wa Chuo Kikuu cha Didoma ambaye pia Mtaalam wa maendeleo ya jamii,Wilayani humo,Dk.Ombeni Msuya alisema kuwa, endapo serikali ikafanya upembuzi yakinifu katika mabwawa na misitu iliyopo Wilaya humo ambayo kwa kiasi kikubwa yameshaulika na kuwashirikisha wananchi itasaidia kukuza pato la mwananchi mmoja mmoja na kuinua uchumi wa Halmashauri.


Dkt Msuya amsema Mabwawa katika Wilaya hiyo hasa bwawa la Kisanjuni limeshaulika kwa muda mrefu lakini serikali na wadau wanaweza kutumia mabwawa haya kwa shughuli za kiuchumi hasa katika kufuga samaki kwa njia za kisasa maana Tanzania tumekuwa na mwamko mkubwa wa ufugaji wa samaki.
Ameongeza kwa kusema uhitaji wa samaki bado ni mkubwa sana,na endapo wananchi watashirikishwa namna ya kufanya ufugaji bora wa samaki itasaidia kuzalisha kwa wingi samaki na itasaidia kukuza uchumi wa Halmashauri yetu na wananchi kwa ujumla.

Mkuu wa Idara ya mifugo na uvuvi ,Emmanuel Sindiyo amesemama Halmashauri ya Wilaya hiyo kupitia ofisi ya mkuu wa wilaya wameandaa mkakati wa kufufua mabwawa katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ili kuwa na uzalishaji mzuri wa samaki na shughuli nyingine za kilimo kandokando ya mabwawa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mgombea urais wa chama tawala Burundi atangazwa mshindi kwa kupata asilimia 68.7

Mgombea urais wa chama tawala nchini Burundi Evariste Ndayishimiye ametangazwa mshindi leo kwenye kinyang’anyiro hicho ambacho kimedaiwa kukumbwa

Read More...

Watu 7 Wanaodhaniwa Kuwa Majambazi Wauawa Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua majambazi saba na kufanikiwa kukamata silaha ndogo Bastola

Read More...

Watanzania watakiwa kucheki afya zao na kufuata ushauri wa daktari.

Watanzania wametakiwa kuwa na mazoea ya kwenda vituo vya afya kucheki afya zao na kuacha dhana ya kutumia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu