Wilshere ajiunga na West Ham.

In Michezo

Mchezaji wa zamani wa Arsenal Jack Wilshere amejiunga na klabu ya West Ham kwa mkataba wa miaka mitatu na kusema kuwa amejiunga na klabu aliyoishabikia akiwa mtoto.

Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 na Arsenal ilikwisha mwisho wa mwezi Juni.

Najihisi mtu maalum . Wengi wanajua kwamba nimekuwa na uhusiano mkubwa na klabu hii wakati wote nilipokuwa mtoto nikiwatizama wakicheza katika uwanja wa Upton Park

Klabu hiyo pia inakaribia kumsajili mshambuliaji wa Ukraine Andriy Yarmolenko. Tayari dau la yuro milioni 20 limekubaliwa na klabu ya Ujerumani Borussia Dortmund.

Wilshere anatarajiwa kujiunga na kikosi cha mkufunzi mpya wa klabu hiyo Manuel Pellegrini nchini Switzerland ambapo klabu hiyo imekita kambi ikifanya mazoezi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

PICHA:Rais Magufuli akitoa salamu za pole familia ya Kikwete

Kufuatia kifo cha Rashid Mkwachu ambaye ni Baba mzazi wa mke wa Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, mama Salma

Read More...

Lugola awapa maagizo wakuu wa majeshi, Wafungwa watumie nguvu zao kujitaftia chakula.

Waziri wa mambo ya Ndani, Kangi Lugola mapema leo hii ameongea na vyombo vya habari akiwasilisha maagizo mbalimbali ambayo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu