Yafahamu makundi ya leseni za udereva.

In Tekinolojia

Mfumo wa leseni za udereva utakuwa na makundi mbalimbali ya madaraja ya leseni za udereva kama ifuatavyo:

Pikipiki

A – Leseni ya kuendesha pikipiki zenye/zisizo na kigari na ambazo injini zake zina ukubwa zaidi ya cc 125 au uzito wa kilo 230.

A1 –  Leseni za kuendesha pikipiki  zisizo na kigari na ambazo ukubwa wake wa injini ni mdogo kuliko cc 125 au chini ya kilo 230.

A2 – Leseni ya kuendesha pikipiki za magurudumu matatu na  manne.

A3 – Leseni za kuendesha pikipiki baiskeli ambazo ukubwa wake wa injini hauzidi cc 50

Vyombo Binafsi vya Moto

B – Leseni ya kuendesha aina zote za vyombo vya moto isipokuwa pikipiki, magari ya biashara, magari makubwa na magari ya kutoa huduma kwa umma.

Magari ya kutoa huduma kwa Umma

C – Leseni ya kuendesha magari ya kutoa huduma kwa umma yenye uwezo wa kubeba abiria 30 na zaidi pamoja na dereva. Magari katika kundi hili yanaweza kufungwa tela lenye ujazo wa juu unaokubalika usiozidi kilo 750. Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na leseni ya daraja CI au E kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.

C1 – Leseni ya kuendesha magari ya kutoa huduma kwa umma yenye uwezo wa kubeba abiria 15 lakini wasiozidi 30, abiria pamoja na dereva. Magari katika kundi hili yanaweza kufungwa tela lenye ujazo wa juu unaokubalika usiozidi kilo 750. Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na leseni ya daraja D kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.

C- Leseni za kuendesha magari ya kutoa huduma kwa umma yenye uwezo wa kubeba abiria wanne lakini wasiozidi kumi na tano. Magari katika kundi hili yanaweza kufungwa tela lenye ujazo unaokubalika usiozidi kilo 750. Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na leseni ya daraja D kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.

C3 – Leseni za kuendesha magari ya kutoa huduma kwa umma yenye uwezo wa kubeba abiria wanne au pungufu akiwemo dereva. Magari katika kundi hili yanaweza kufungwa tela lenye ujazo unaokubalika usiozidi kilo 750. Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na leseni ya daraja D kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.

Magari Madogo ya Mizigo ya Biashara

D – Leseni ya kuendesha aina zote za vyombo vya moto isipokuwa pikipiki, magari makubwa na magari ya kutoa huduma kwa umma.

Magari makubwa ya Mizigo ya biashara

E – Leseni ya kuendesha aina zote za vyombo vya moto isipokuwa pikipiki na magari ya umma. Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na leseni ya daraja D kwa muda usiopungua miaka mitatu.

Magari yenye Trela

F – Leseni ya kuendesha magari yanayokokota trela.

Magari ya Shambani na Migodini

G – Leseni ya kuendesha magari ya shambani na migodini.

Wanaojifunza

H – Leseni ya muda ya kujifunza

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu