YANGA KUMLIPA YANGA

In Michezo

Muda mfupi baada ya kuwapo kwa taarifa kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuwa imeifungia Yanga kusajili misimu mitatu kwa kushindwa kumlipa mchezaji wake wa zamani, Amis Tambwe deni la Sh milioni 41, klabu hiyo imeahidi kuweka mambo sawa. Tambwe aliyeitumikia Yanga kwa zaidi ya misimu miwili iliyopita, amesema anaidai klabu hiyo fedha zake za usajili na mishahara.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali jana zilieleza kuwa, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Dk Mshindo Msolla hana shida juu ya hilo na ameahidi kulipa deni hilo kama ilivyotokea kwa wengine waliokuwa wanadai huko nyuma.

“Tuna utaratibu wetu wa kulipa madeni na FIFA wana ufahamu tunalipa nusu nusu na hata George Lwandamina na Mwinyi Zahera tuliwalipa hivyo na Tambwe atalipwa kwa utaratibu huo,” alisema. Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Hersi Said alisema ndani ya wiki hii watahakikisha wanakamilisha deni hilo.

Aliwataka mashabiki na wanachama wa Yanga kutokuwa na wasiwasi kwani wapo imara kuijenga klabu hiyo ndani na nje ya uwanja kwa kuwapa kilicho bora. Awali, Wakili wa Tambwe, Felix Majani alisema Yanga ikikamilisha deni hilo itafunguliwa kifungo hicho na kuendelea na utaratibu wa kawaida. Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Ismail Rage alihimiza klabu hiyo kuheshimu mikataba ya wachezaji wao.

Alisema Yanga wanatakiwa kulipa fedha hizo haraka iwezekanavyo na kadiri wanavyochelewa wanaweza kuingia kwenye hatari ya kuondolewa kwenye mashindano ya aina yoyote ya kimataifa na hata kuigharimu timu ya taifa kutoshiriki mashindano ya Afrika baadaye

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Wananchi Wa Siha Washukuru Serikali Kukabiliana na Nzige

Wananchi wa wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro wameipongeza serikali kwa hatua iliyochukua kudhibiti makundi ya nzige waliovamia maeneo

Read More...

Wizara Ya Afya Yawataka Wananchi Kuchukua Tahadhari Dhidi ya COVID – 19

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewasihi na kuwasisitiza zaidi wananchi kuzingatia tahadhari zote ikiwemo

Read More...

Ndege mbili kupambana na nzige Longido

Serikali nchini imetangaza kuanza kutumia ndege kunyunyizia dawa makundi ya nzige yaliyovamia wilaya ya Longido na Simanjiro wakitokea

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu