YANGA YAPIGWA FAINI YA MIL 3

In Kitaifa, Michezo

Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) imeitoza Timu ya Young Africans SC faini ya sh. 3,000,000 (milioni tatu) kwa makosa yafuatayo:-

▪️Kutumia mageti ya uwanja wa Uhuru kuingia uwanja wa Benjamin Mkapa badala ya mlango maalum unaotumiwa na timu

▪️ Kutumia mlango wa chumba cha waandishi wa habari (media center) badala ya mlango maalum unaotumiwa na timu

▪️Kuingia uwanjani kupasha misuli (warm up) kwa kutumia mlango (Gate B) ambao haukupangwa kutumika kwa namna yoyote

▪️Kutumia chumba cha wafanya usafi wa uwanja kwa ajili ya kubadilisha nguo badala ya chumba maalum cha kubadilishia nguo (Dressing Room).

Pia timu ya Young Africans SC inatakiwa kulipa Tsh. 850,000/= ikiwa ni gharama ya ukarabati wa mageti yaliyovunjwa wakati wa wakiingia uwanjani pamoja na makufuli ya uwanja wa Benjamin Mkapa yaliyoharibiwa katika tukio hilo

Matukio hayo yalitokea katika mchezo wa Watani wa Jadi uliochezwa Julai 3, 2021 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na Kumalizika kwa Yanga kuibuka na Alama 3 kufuatia Ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Simba Sc.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu