Yesu Bandia hakufariki na bado yupo Kenya.

In Kimataifa

Mhubiri wa Marekani na muigizaji Michael Job, ambaye hivi karibuni alikuwa nchini Kenya na kuitwa ‘Yesu bandia’ hajafariki kama ilivyotangazwa hapo jana na vyombo vya habari na mitandao.

Kulingana na uchunguzi wa BBC Swahili Mhubiri huyo yupo hai na mzima wa afya, pia yupo nchini Kenya na kwamba hajatimuliwa kama ilivyodaiwa awali.
Taarifa za vyombo vya habari zilianza kuenezwa kuwa,Yesu huyo bandia alifariki siku chache tu baada ya kuhudhuria ibada ya kidini.
Hata hivyo mhubiri huyo ameendelea kuchapisha picha na video za shughuli zake siku baada ya siku.

Katika chapisho hilo na kanda za video alizoweka katika akaunti yake ya facebook, Bwana Job anaonekana katika gari moja akihubiri Kiingereza huku akisaidiwa na mkalimani huku watu wakifuatilia mahubiri yake.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE

Real Madrid bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili Neymar, lakini wanataka hakikisho kutoka Paris St-Germain kuhusu hali

Read More...

(TAMISEMI) KUTOA TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani S Jafo kesho tarehe 23 Mwezi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu