ZAIDI YA MILIONI 200 ZIMETOLEWA KWA AJILI YA KUREKEBISHA MIUNDOMBINU YA BARABARA KATIKA KATA YA MURIETI JIJINI ARUSHA

In Kitaifa

ZAIDI YA MILIONI 200 ZIMETOLEWA KWA AJILI YA KUREKEBISHA MIUNDOMBINU YA BARABARA KATIKA KATA YA MURIETI JIJINI ARUSHA  DIWANI WA KATA YA MURIETI FRANSIS MBISE AMEZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI NA KUELEZEA HALI HALISI


Akizungumza na vyombo vya habari Diwani wa kata ya Muriet jijini Arusha Mh. Frances Mbise amesema kuwa,  kata ya Murieti ni kata ambayo ina mkusanyiko mkubwa wa watu kuliko kata zote na mvua zilizonyesha ziliharibu sehemu mbalimbali jambo linalopelekea wananchi kushindwa kufanya shughuli zao
Amesema kutokana na hayo basi serikali imeanza kuifanyia marekebisho baaddhi ya maeneo kama barabara ya Bon site, Kwa patel, Nabosoito, na sehemu mbalimbali ambapo wamekuwa kipaombe kushirikiana na serikali ili kuweza kuleta maendeleo

Amesema kuwa utekelezaji huo umeshaanza ambapo marekebisho ya barabara bado yanaendea na kuna baadhi ya maeneo wameweka vifusi ili kuweza kupisha wananchi kuendelea na majukumi
“Tunaishukutu serikali ya awamu ya tano kwa kuwajali wananchi wake kwani wametoa fedha hizo kwa ajili ya mapenzi ya kweli na wananchi wake na changamoto kubwa ni ujenzi kusitishwa kutokana na mvua zinazoendea kunyesha na kusitisha ujenzi lakini ujenzi huo utakamilika mvua zikipungua” amesema Mh Mbise


Pia amechukua fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi kutokana na janga la corona kujitahidi kuzingatia kanuni na elimu zinazotolewa na wadau wa afya namna ya kujikinga ikiwa ni pamoja na kuepukana na misongamano isiyo ya ulazima

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mgombea urais wa chama tawala Burundi atangazwa mshindi kwa kupata asilimia 68.7

Mgombea urais wa chama tawala nchini Burundi Evariste Ndayishimiye ametangazwa mshindi leo kwenye kinyang’anyiro hicho ambacho kimedaiwa kukumbwa

Read More...

Watu 7 Wanaodhaniwa Kuwa Majambazi Wauawa Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua majambazi saba na kufanikiwa kukamata silaha ndogo Bastola

Read More...

Watanzania watakiwa kucheki afya zao na kufuata ushauri wa daktari.

Watanzania wametakiwa kuwa na mazoea ya kwenda vituo vya afya kucheki afya zao na kuacha dhana ya kutumia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu