Zitto Kabwe achukizwa na kitendo cha nchi kuagiza mafuta nje.

In Siasa

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa haiingii akilini kwa serikali kuagiza malighafi za kujengea reli nchini, wakati tuna makaa ya mawe na chuma wilayani Ludewa, ambayo mpaka sasa hayajaanza kuchimbwa.

Amesema kuwa serikali ingechukua hatua katika kutengeneza kiwanda cha chuma kutokana na madini ya chuma yaliyopo Ludewa, serikali isingeingia gharama ya kuagiza malighafi za ujenzi wa reli nje, na pia ingeweza kupata kipato kwa kuuza kwa nchi jirani kama Kenya na Zambia, ambako nako kuna ujenzi wa reli unaendelea.

“Kweli inaingia akilini tuna chuma na makaa ya mawe yamejaa pale Ludewa, tunampa mkandarasi kazi ya kujenga reli, vyuma vinatoka Uturuki, India, China kweli Mh. Spika!!? Kenya nao wanajenga reli tungeweza kuwauzia,”amesema Zitto

Hata hivyo, Zitto Kabwe amesema kuwa nchi inatia aibu kuagiza mafuta kutoka nje na kuibua mogoro mkubwa kuhusu bidhaa hiyo, wakati nchi ina rasilimali za kutosha za kutengeneza mafuta, ila haijaweka mikakati wala mipango yoyote kukuza sekta hiyo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu