Zuio lawekwa kwa Sekondari za Azania, Jangwani na Milambo kufunguliwa kesho.

In Kitaifa
Serikali imelazimika kusogeza mbele tarehe ya kufungua shule kwa shule za Azania, Jangwani na Milambo kutokana na Wakala wa Majengo(TBA), kushindwa kumaliza ukarabati huo kwa muda uliotakiwa.
Uamuzi huo ulifikiwa jana  Jumamosi jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Leonard Akwilapo alipokutana na walimu wa shule hizo na viongozi wa Manispaa ya Ilala.
Akwilapo alisema kitendo hicho hakijamfurahisha na kuahidi kufuatilia kwa mara nyingine mkataba wa namna ya utekelezaji wa ukarabati huo walioingia Wizara na TBA.
“TBA mnapaswa kujua mmepewa jukumu hili kwa kuwa Serikali imewaamini, lakini hii isiwe kisingizio cha nyie kuvurunda kwa kisingizio tu ni taasisi ya Serikali nitapitia tena upya na mwanasheria wetu mkataba tulioingia kuona ni wapi watu hawakutekeleza wajibu wao na hatutasita kuchukua hatua tutakapobaini kuna tatizo,” alisema.
Hata hivyo, alisema pamoja na kuongeza siku hizo ambapo sasa badala ya kufungua shule kesho Jumatatu, watafungua Januari 22, hataongeza siku zaidi na kuwahakikishia walimu kwamba muda walioupoteza wa ratiba za kufundisha zitafidiwa katika likizo ya Aprili na ile ya Juni.
Akijibu sababu zilizowachelewesha kumaliza ukarabati huo kwa muda, Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Dar es Salaam,  Manasseh Shekalaghe alisema zipo sababu nyingi zilizochelewesha ikiwemo gharama kuongezeka tofauti na ilivyodhaniwa awali.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu